-
SADC yaitisha mkutano wa dharura kuhusu mgogoro wa Msumbiji
Nov 07, 2024 03:29Ghasia za baada ya uchaguzi nchini Msumbiji kufuatia mzozo wa uchaguzi wa Oktoba 9 zimesababisha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuitisha mkutano wa dharura mjini Harare wiki ijayo.
-
Somalia yaitaka Ujerumani isiwafukuze wahajiri Waafrika
Nov 07, 2024 03:03Somalia imeitaka Ujerumani isitishe mpango wake wa kuwafukuza Waafrika wakiwemo Wasomali nchini humo.
-
Amnesty International yaitaka Mali ifanye uchunguzi wa vifo vya raia katika mashambulio ya droni
Nov 06, 2024 22:59Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za binadamu la Amnesty International, limeiitaka serikali ya Mali kufanya uchunguzi kuhusiana na mauaji ya raia wanane, wakiwemo watoto wadogo waliouawa katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.
-
Kenya yaomba msaada wa China kujiunga na BRICS
Nov 06, 2024 10:02Rais wa Kenya William Ruto ameomba China iunge mkono ombi la taifa hilo la Afrika Mashariki kujiunga na kundi hilo BRICS.
-
Baraza la Kiislamu la Msumbiji lajitolea kupatanisha baina ya serikali na waasi
Nov 06, 2024 07:33Baraza la Kiislamu la Msumbiji limejitolea kuwa mpatanishii kati ya serikali na waasi wanaopigana na serikali katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado katika taifa hilo la kusini mwa Afrika.
-
Watoto 36 wapoteza maisha kwa malaria Sudan Kusini katika muda wa wiki 2
Nov 05, 2024 22:59Afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Sudan Kusini jana Jumanne alithibitisha kupoteza maisha watu 41 kutokana na ugonjwa wa malaria ,36 wakiwa ni watoto katika mji wa Pibor nchini humo.
-
UN: Milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini imeuwa watu 16 Libya tangu kuanza mwaka huu
Nov 05, 2024 22:48Watu 16 wakiwemo watoto wadogo wamepoteza maisha huko Libya tangu kuanza mwaka huu wa 2024 kufuatia milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini na masalia ya zana za vita ambazo hazikulipuka.
-
Mali yaungana na makumi ya nchi za Afrika kujinaisha vitendo vya ufuska vya 'ushoga'
Nov 05, 2024 09:15Bunge la Mpito la Mali limepitisha sheria inayojinaisha vitendo vya ufuska vya 'ushoga' na kujiunga na makumi ya nchi zingine za Kiafrika zilizopitisha sheria ya kupiga marufuku vitendo hivyo vinavyotetewa na Ulimwengu wa Magharibi kwa kisingizio cha haki za binadamu.
-
DRC: Waasi wa M23 wauteka mji mpya kwenye mpaka na Uganda huku mazungumzo yakijivuta
Nov 05, 2024 03:57Waasi wa M23 wanaendelea kupata nguvu mashariki mwa DRC.
-
Sudan sasa yakumbwa na kipindupindu na homa ya kidingapopo
Nov 04, 2024 22:52Nchini Sudan ambako vita na janga la njaa vinaendelea kuwahangaisha raia sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo (dengue) huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani.