-
Wahifadhi Qur'ani Tukufu nchini Nigeria waitaka serikali kuiunga mkono Palestina
Nov 04, 2024 09:25Jukwaa la Huffadh wa Qur'ani Tukufu la Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria, limeandaa kongamano la siku mbili Jumamosi na Jumapili katika mji wa Potiskum wa Jimbo la Yobe Kaskazini Mashariki, ili kusisitiza uungaji mkono kwa mhimili wa muqawama ambao unapigana dhidi ya utawala katili wa Israel na pia kuwaombea dua mashahidi.
-
Radi yaua na kujeruhi watu 48 kanisani, kaskazini mwa Uganda
Nov 04, 2024 02:57Watu 14 wamepoteza maisha na wengine 34 wamejeruhiwa baada ya radi kupiga kanisani wakati watu walipokuwa wamekusanyika humo kufanya maombi, kaskazini mwa Uganda.
-
Ethiopia yazishutumu balozi za kigeni kwa kuvuruga uchumi, yatishia kuchukua hatua
Nov 04, 2024 02:57Waziri Mkuu wa Ethiopiam, Abiy Ahmed amezishutumu balozi za kigeni kwa kujihusisha na magendo ya fedha za kigeni akidai kuwa balozi hizo zinaibia Ethiopia rasilimali zake.
-
Serikali ya Sudan yapeleka msaada wa matibabu katika maeneo yenye vita
Nov 03, 2024 22:54Wizara ya Afya ya Sudan imetangaza kwamba imepeleka vifaa vya dharura vya matibabu katika mikoa iliyoathiriwa na mgogoro wa vita unaendelea hivi sasa nchini humo.
-
Niger yasaini makubaliano ya ushirikiano wa satelaiti 3 na kampuni moja ya Russia
Nov 03, 2024 22:53Serikali ya Niger, ikiwakilishwa na Waziri wa Mawasiliano, Sidi Mohamed Raliou, imetia saini makubaliano ya kushirikiana na shirika moja la Russia katika kuendesha satelaiti tatu.
-
Machafuko yaendelea kushuhudiwa Msumbiji
Nov 03, 2024 08:12Polisi nchini Msumbiji imetumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji katika miji kadhaa ya nchi hiyo waliokuwa wakiandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wenye utata.
-
RSF yaendeleza hujuma za umwagaji damu Sudan
Nov 03, 2024 03:13Kwa akali watu 18 wameuawa na wengine watano wamejeruhiwa katika mashambulizi mawili tofauti ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika jimbo la Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudan.
-
Jeshi la Nigeria laua 'magaidi' 187 ndani ya wiki moja
Nov 03, 2024 02:46Zaidi ya watu 187 wanaoshukiwa kuwa magaidi wameuawa huku wengine 262 wakikamatwa katika operesheni mbalimbali za kupambana na ugaidi za jeshi la Nigeria nchini kote katika muda wa wiki moja iliyopita.
-
Chad yakanusha kuwaua raia katika mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo
Nov 02, 2024 23:40Serikali ya Chad imekanusha vikali ripoti kwamba jeshi lake liliwashambulia raia katika operesheni dhidi ya wanamgambo wanaobeba silaha.
-
WHO: Zaidi ya watu 50,000 wamepata chanjo ya Mpox Kongo na Rwanda
Nov 02, 2024 23:03Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, zaidi ya watu 50,000 kufikia sasa wamechanjwa dhidi ya virusi vya mpox katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda.