-
Msemaji wa M23 auawa katika shambulio la droni mashariki mwa DRC
Feb 24, 2026 22:54Msemaji wa waasi wa M23 ameripotiwa kuuawa katika shambulio la ndege isiyo na rubani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Madagascar: Ushirikiano wetu na BRICS utatupa fursa mpya
Feb 24, 2026 22:54Rais wa mpito wa Madagascar, Michael Randrianirina amesema kwamba, nchi hiyo inatazama ushirikiano na jumuya ya BRICS kama njia ya kuelekea kwenye fursa mpya za kiuchumi na ushirikiano wa kimataifa.
-
Mwana wa Rais wa Uganda amuita 'Hitler' kiongozi wa RSF aliyekutana na baba yake hivi karibuni
Feb 24, 2026 07:43Mwana mtatanishi wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye ni mkuu wa majeshi ya nchi hiyo Muhoozi Kainerugaba ametoa matamshi yasiyo ya kawaida katika kumshambulia kiongozi wa wanamgambo wa Sudan wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF), Mohamed Hamdan Dagalo ambaye hivi karibuni alikutana na baba yake huko nchini Uganda.
-
Afrika Kusini: Tutafuta zaidi ya viza 2,000 zilizotolewa kupitia mitandao ya rushwa
Feb 24, 2026 07:41Afrika Kusini inajiandaa kufuta zaidi ya viza 2,000 ambazo zimepatikana kwa njia isiyo sahihi, huku serikali ikiendesha msako mkali wa kupambana na rushwa ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
-
Kwa nini Somaliland imeipa ofa Marekani ya kuanzisha kituo cha kijeshi katika ardhi yake?
Feb 24, 2026 05:09Somaliland imeipa Marekani ofa na fursa ya kuanzisha kambi ya kijeshi katika ardhi yake. Vyanzo vya habari vimeripoti kwamba, maafisa wa Somaliland wameipa Washington ofa ya kutumia rasilimali za madini za eneo hilo na kuanzisha kambi ya kijeshi.
-
Afrika Kusini yatoa wito kwa nchi wanachama wa UN kulitambua taifa la Palestina
Feb 24, 2026 04:31Afrika Kusini jana Jumatatu ilitoa wito kwa nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa kulitambua taifa la Palestina na kudhihirisha mshikamano na wananchi wa Palestina.
-
Sudan: Pendekezo lolote la kumaliza vita linapasa kulinda maslahi ya taifa na umoja wa ardhi ya nchi hiyo
Feb 24, 2026 04:30Sudan imesema kuwa pendekezo lolote la kumaliza vita na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) linapasa kuzingatia maslahi makuu ya nchi hiyo, mshikamano na umoja wa ardhi nzima ya nchi hiyo.
-
Wanamgambo wanaoiunga mkono serikali: Tumewauwa wapiganaji 50 wa M23 mashariki mwa Kongo
Feb 24, 2026 04:29Wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamedai kuwa wamewauwa wapiganaji 50 waliokuwa wanachama wa kundi la waasi wa M23 na kuwateka nyara kadhaa katika mapigano makali hivi karibuni.
-
Machungu ya Ukoloni | Eritrea: Chini ya kivuli cha apathaidi ya Italia, simulizi ya udhalilishaji na mapambano
Feb 24, 2026 00:37Ukandamizaji wa kikoloni wa Italia nchini Eritrea haukuwa tu mradi wa upanuzi wa ushawishi wa kisiasa, bali ulikuwa mfumo uliosimikwa juu ya uvamizi wa kijeshi, ubaguzi wa rangi au apathaidi, ukandamizaji wa upinzani, na utumwa. Mfumo huu wa kikoloni ulifikia kilele mwaka 1938, katikati ya jiji la Roma, hatua ya malalmiko iliyochukuliwa na Zerai Deres ilipofichua wazi unafiki na ukatili wa utawala huo.
-
Chad yatangaza kufunga mpaka wake na Sudan kuzuia kuenea mapigano mpakani mwake
Feb 24, 2026 00:35Chad imetangaza kuwa, ili kuzuia kuenea mapigano kwenye maeneo ya mpakani, inaufunga mpaka wake wa pamoja na Sudan hadi itakapotolewa taarifa nyingine.