-
Guterres: UN inafuatilia hali ya Guinea-Bissau 'kwa wasiwasi mkubwa' baada ya jeshi kufanya mapinduzi
Nov 26, 2025 23:27Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa anafuatilia matukio ya Guinea Bissau kwa wasiwasi mkubwa baada ya baada ya jeshi la nchi hiyo jana Jumatano kumuondoa madarakani Rais Umaro Sissoco Embalo wa nchi hiyo.
-
OXFAM: Nusu ya raia Sudan Kusini wanakabiliwa na njaa kali
Nov 26, 2025 22:59Shirika la OXFAM limetangaza kuwa, takriban watu milioni sita wanakabiliwa na baa la njaa kali Sudan Kusini, idadi ambayo ni sawa na nusu ya raia wote nchini humo.
-
Gavana wa Darfur: Katika kipindi cha siku tatu tu, RSF iliua Wasudan 27,000 El-Fasher
Nov 26, 2025 07:21Gavana wa Jimbo la Darfur nchini Sudan, Minni Arko Minnawi, ameviambia vyombo vya habari kuwa, katika kipindi cha siku tatu tu Wasudan 27,000 waliuliwa na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) wakati wanamgambo wa vikosi hivyo walipoendeleza wimbi la mauaji baada ya kuuteka mji wa el-Fasher mwishoni mwa mwezi uliopita.
-
UN: Tangazo la RSF la kusitisha mapigano ni 'hatua katika mwelekeo sahihi'
Nov 26, 2025 03:43Umoja wa Mataifa umekaribisha kwa tahadhari tangazo la kibinadamu la kusitisha mapigano lililotolewa jana na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), ukisema kuwa linawakilisha kupiga hatua lakini linahitaji kuidhinishwa kupitia hatua maidanini.
-
Rais wa Nigeria: Wanafunzi wa kike 24 waliotekwa nyara wiki jana wakombolewa
Nov 26, 2025 03:43Wanafunzi wa kike 24 waliokuwa wametekwa nyara kutoka katika shule yao ya bweni wiki iliyopita kaskazini magharibi mwa Nigeria wamekombolewa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais.
-
Russia: Tupo tayari kuisaidia Nigeria katika mapambano dhidi ya ugaidi
Nov 26, 2025 03:42Maria Zakharova Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa nchi hiyo ipo tayari kusaidia na kuung amkono juhudu za nigeria za kupambana na ugaidi. Bi Zakharova aidha amepongeza jitihada kubwa za serikali ya Abuja za kukabiliana na makundi yenye misimamo mikali.
-
Wakuu wa usalama Nigeria waripoti maendeleo katika operesheni ya kuokoa wanafunzi waliotekwa nyara
Nov 25, 2025 03:59Maafisa wa jeshi la Nigeria wametangaza kuwa kumepigwa hatua nzuri za maenedelea katika jitihada za kukomboa mamia ya wanafunzi wa kike na walimu wao kadhaa waliotekwa nyara na kundi la watu waliokuwa na silaha katika jimbo la Niger, kaskazini mwa nchi hiyo.
-
Hemedti atangaza kusitisha mapigano kwa upande mmoja, raia wanaendelea kukimbia makazi yao Sudan
Nov 25, 2025 03:09Kamanda wa waasi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), Mohamed Hamdan Dagalo “Hemedti”, ametangaza kusitisha mapigano ya ndani kwa kipindi cha miezi mitatu kwa "sababu za kibinadamu", ambako kunajumuisha kusitishwa uhasama; siku moja baada ya mkuu wa Baraza la Mpito la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, kukaataa pendekezo la Marekani kwa ajili ya kusitisha mapigano.
-
IEBC yawataka wanasiasa wa Kenya wasichochee machafuko na uvunjivu wa amani
Nov 25, 2025 03:04Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), imewataka wanasiasa kuelekeza nguvu zao katika kuhimiza amani na utulivu, badala ya kutoa matamshi yanayoweza kuchochea taharuki miongoni mwa wananchi.
-
Familia za watoto waliotekwa nyara Nigeria zachanganyikiwa kutokana na kukaririwa vitendo hivyo mashuleni
Nov 24, 2025 23:13Familia za wanafunzi waliotekwa nyara nchini Nigeria zimenasa kati ya matumaini na kukatishwa tamaa kutokana na vitendo vya kukaririwa vya utekaji nyara wanafunzi wakiwa mashuleni.