-
Hamas: Kitendo cha utawala wa Kizayuni kukataa kukabidhi miili ya mashahidi wa Kipalestina kinaonyesha ukatili
Aug 27, 2025 12:49Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeashiria kuwa, utawala ghasibu wa Israel umekataa kukabidhi maiti 726 za mashahidi wa Kipalestina na kukitaja kitendo hicho kuwa jinai na ukatili wa kutisha wa adui Mzayuni.
-
Sisitizo la Malaysia juu ya uungaji mkono endelevu kwa Palestina
Aug 27, 2025 12:47Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Malaysia amesema kuwa, nchi hiyo itadhibiti na kusimamia vilivyo vitisho au ugaidi wowote unaohusiana na suala la uungaji mkono wa Kuala Lumpur kwa Palestina na kuwa itadumisha misimamo ya kuwaunga mkono Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni.
-
Abbas Araghchi: Wakaguzi wa IAEA wanaingia nchini kwa uamuzi wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa
Aug 27, 2025 12:44Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuingia nchini kwa wakaguzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA ni uamuzi uliochukuliwa na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa kwa ajili ya kuchunguza suala la kubadilishwa mafuta ya kiwanda cha kuzalisha umeme cha Bushehr. Amesema hakuna maafikiano yoyote yaliyofikiwa kuhusu ushirikiano mpya wa Iran na wakala huo.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel akiri kutengwa utawala huo kisiasa
Aug 27, 2025 12:42Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kutengwa na kuzingirwa kisiasa utawala huo katika ngazi za kimataifa.
-
Afisa mkuu wa Hezbollah nchini Lebanon: Muqawama hauwezi kusalimu amri
Aug 24, 2025 11:56Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah huku akisisitiza kuwa, uamuzi wa serikali ya Lebanon wa kuupokonya silaha muqawama ni uamuzi usio wa kisheria wala halali amesema: Muqawama ni utamaduni na utambulisho usioweza kutokomezwa.
-
Pongezi za Kamati za Muqawama wa Palestina/Yemen yafanyia majaribio kombora jipya dhidi ya Israel
Aug 24, 2025 11:53Katika shambulio lake la Ijumaa usiku Yemen ilifanyia majaribio kwa mafanikio kombora jipya dhidi ya adui Mzayuni, jambo ambalo lilizifurahisha sana kamati za muqawama wa Palestina na kuzifanya ziwashukuru watu wa Yemen kwa mafanikio hayo.
-
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa: Ni wakati wa kuchukua hatua; tunahitaji usitishaji mapigano mara moja Gaza
Aug 24, 2025 12:02Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema kuhusiana na tangazo rasmi la mgogoro wa baa la njaa huko Gaza, kwamba anaamini kuwa sasa ni wakati wa kuchukuliwa hatua na kwamba usitishaji mapigano unapasa kutekelezwa mara moja na misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kuingia katika ukanda huo bila masharti wala vikwazo vyovyote.
-
Kukanusha kukaribia kusainiwa makubaliano ya usalama kati ya serikali ya mpito ya Syria na utawala wa Israel
Aug 24, 2025 11:59Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya serikali ya mpito ya Syria siku ya Jumamosi ilikanusha habari iliyochapishwa kuhusu kukaribia kusainiwa kwa makubaliano ya usalama kati ya Damascus na utawala wa Kizayuni.
-
Sisitizo la Iran na China la kuimarisha na kuharakisha ushirikiano wa kielimu na kiteknolojia
Aug 21, 2025 07:51Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Ushirikiano wa Kielimu na Kiteknolojia la Iran amegusia historia angavu na ya kirafiki ya uhusiano kati ya Iran na China na kusisitiza haja ya kupanuliwa na kuharakishwa ushirikiano wa kielimu na kiteknolojia kati ya nchi mbili.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri: Mpango wa nyuklia wa Iran hauna suluhisho la kijeshi
Aug 21, 2025 08:10Katika mazungumzo yake ya simu na Steve Wittkoff, Mjumbe wa Rais wa Marekani katika Masuala ya Asia Magharibi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesisitiza juu ya ulazima wa kupunguzwa mivutano katika eneo hili na kusema kuwa, mpango wa nyuklia wa Iran hauna suluhisho la kijeshi.