Sisitizo la Malaysia juu ya uungaji mkono endelevu kwa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i130072-sisitizo_la_malaysia_juu_ya_uungaji_mkono_endelevu_kwa_palestina
Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Malaysia amesema kuwa, nchi hiyo itadhibiti na kusimamia vilivyo vitisho au ugaidi wowote unaohusiana na suala la uungaji mkono wa Kuala Lumpur kwa Palestina na kuwa itadumisha misimamo ya kuwaunga mkono Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni.
(last modified 2025-08-27T12:48:59+00:00 )
Aug 27, 2025 12:47 UTC
  • Sisitizo la Malaysia juu ya uungaji mkono endelevu kwa Palestina

Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Malaysia amesema kuwa, nchi hiyo itadhibiti na kusimamia vilivyo vitisho au ugaidi wowote unaohusiana na suala la uungaji mkono wa Kuala Lumpur kwa Palestina na kuwa itadumisha misimamo ya kuwaunga mkono Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Mohammad Alamin, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia ameongeza kuwa: "Msimamo wa nchi hii kuhusu Palestina umekuwa thabiti kwa miongo kadhaa na inawaunga mkono Wapalestina." Amesema kwenye ukumbi wa Bunge la Malaysia kwamba: "Kuhusu vitisho au ugaidi unaoweza kufanywa dhidi yetu kwa kuunga mkono suala la Palestina, ninaamini hili ni jambo ambalo tunaweza kulidhibiti kwa sababu msimamo wetu katika suala hili ni imara."