Israel, tishio kwa amani na usalama wa eneo la Asia Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i136776-israel_tishio_kwa_amani_na_usalama_wa_eneo_la_asia_magharibi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa: Utawala wa Kizayuni wa Israel umefanya jinai kubwa zaidi kwa kupewa kinga kamili katika kipindi cha miongo minane iliyopita.
(last modified 2026-02-18T11:19:53+00:00 )
Feb 18, 2026 11:19 UTC
  • Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
    Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa: Utawala wa Kizayuni wa Israel umefanya jinai kubwa zaidi kwa kupewa kinga kamili katika kipindi cha miongo minane iliyopita.

Sayyid Abbas Araqchi amesema katika hotuba yake katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya mjini Geneva, Uswisi kwamba: Katika kipindi cha chini ya miaka miwili Israel imezishambulia nchi saba za eneo la Magharibi mwa Asia na kuua zaidi ya watu 70,000 huko Gaza katika fremu ya mfumo wa mauaji ya kimbari ya kikoloni. "Hakuna jinai ambayo haijafanywa na utawala huu, na hakuna mstari mwekundu ambao haujavukwa na Israel", amesema Araqchi.

Ameongeza kuwa: Katika hali ambayo Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zinapuuza vitisho vya utawala ghasibu wa Israel kwa amani na usalama wa dunia ukiwemo uwezo wake wa nyuklia, zinaendelea kudai kuwa miradi ya nyuklia ya Iran inayofanywa kwa malengo ya amani na kwa ajili ya matumizi ya kiraia ni tishio kwa amani na usalama wa kimataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Kinachotia wasiwasi sana ni kukimbilia kuishambulia kijeshi Iran mwezi Juni mwaka jana; tena wakati ambapo tulikuwa tukiendelea na mazungumzo. Hatua hiyo inakinzana waziwazi na kanuni kuu za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.

Araqchi amesema kuwa: Marekani ilishirikiana na dola lisilo mwanachama wa mkataba wa NPT dhidi ya nchi ambayo ni mwanachama wa mkataba huo na kutoa kusababisha madhara kwa umoja wa ardhi ya nchi, hadhi na uhai wa makataba huo. Mashambulizi dhidi ya vituo vya nyuklia ambavyo vilikuwa vikifanya shughuli zake chini ya uangalizi wa wakala wa IAEA yanaweza kutajwa kama jinai ya kivita, hatua ambayo inaweza kusababisha hatari ya kuvuja kwa miale ya radioactive, kuchafua mazingira kwa muda mrefu na kuenea athari mbaya katika eneo zima. 

Israel haijasaini Mkataba wa NPT

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Kushindwa  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) kulaani vikali mashambulizi hayo kumeacha rekodi ya hatari katika historia.

Utawala wa Kizayuni wa Israel uliasisiwa kwa msingi wa uvamizi na kukalia kwa mabavu ardhi za mataifa mengine na sera za kupenda kujitanua. Vitendo vya uchokozi na kijeshi vya Israel vinavyoshuhudiwa kila uchao katika nchi mbalimbali za kanda hii ikiwa ni pamoja na Lebanon, Syria, Iraq, Iran, na hasa katika Ukanda wa Gaza vinaonyesha wazi chanzo cha ukosefu wa amani na hali ya mchafukoge katika eneo la  Asia Magharibi.

Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa na taasisi za kimataifa; mashambulizi ya mara kwa mara utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza ambayo yamesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya raia wa Palestina. Hujuma hizo zinaonyesha mwenendo wa kimfumo na ulioratibiwa wa mauaji ya kimbari ya utawala huo. Vitendo vyote  hivi vinahesabiwa  kuwa  jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu. Aidha kuendelea kupewa kinga ya kutoshtakiwa na kufuatiliwa kimataifa utawala huo kumeuandalia mazingira ya kuendelea kufanya jinai zaidi bila ya wasiwasi. 

Mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza 

Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya kwa kukosoa sera za undumakuwili  si tu zinafumbia macho hatua za utawala wa Kizayuni, bali zinazuia  hatua yoyote rasmi ya ya kulaaniwa Israel kwa kutumia haki ya kura ya veto ndani ya Baraza la Usalama la UN. 

Mkabala wake, Marekani na washirika wa Magharibi wa White House zinaiarifisha miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya kiraia kuwa tishio kwa usalama wa dunia; katika hali ambayo uwezo wa kijeshi na hata wa kinyuklia wa utawala wa Kizayuni ambao si mwanachama wa NPT, haujawahi kuchunguzwa au kuwekewa vizuizi. Nyendo kama hizi za kibaguzi zinaonyesha namna maslahi ya kisiasa yanavyobinya na kukandamiza haki za mataifa mengine duniani.

Hatua ya kichokozi ya pamoja ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran inahesabiwa kuwa ukiukaji wa wazi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kanuni inayopiga marufuku matumizi ya nguvu. Kitendo kama hiki sio tu ni shambulio kwa nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa, lakini pia kinadhoofisha pakubwa imani ya nchi za dunia kwa Mkataba Unaopiga Marufuku Uenezaji wa Silaha za Nyuklia NPT na viwango vya usalama vya wakala wa IAEA. Tukio hili linaonyesha kwamba mifumo ya kisheria ya kimataifa haina dhamana athirifu ya utekelezaji mkabala wa tawala za Magharibi na washirika wao.