-
Mhariri Mkuu wa Middle East Eye: Harakati ya HAMAS katu haitasalimu amri
Apr 25, 2025 07:23David Hearst, Mhariri Mkuu wa tovuti ya habari ya Middle East Eye amesema, Muqawama ndio njia pekee iliyobaki kwa ajili ya kukomesha ughasibu na kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Serikali ya Jordan yaipiga marufuku harakati kongwe ya Kiislamu ya Ikhwanul-Muslimin
Apr 24, 2025 04:14Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jordan ametangaza kuwa utawala huo wa kifalme umeipiga marufuku harakati ya Kiislamu ya Ikhwanul-Muslimin na kuielezea "itikadi" yake inayohubiri kuwa sasa ni 'haramu' kisheria nchini humo.
-
HAMAS yalitolea wito Baraza Kuu la PLO: Vunjeni uhusiano wenu wa kiusalama na Israel
Apr 24, 2025 04:13Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imelitaka Baraza Kuu la Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO livunje uhusiano wa uratibu wa kiusalama uliopo baina yake na utawala wa Kizayuni na kuchukua msimamo wa pamoja wa Palestina dhidi ya mauaji ya kinyama yanayoendelea huko Ghaza.
-
Kubadilika mtazamo wananchi wa Marekani kuhusu Israel, Palestina na Hamas
Apr 24, 2025 03:31Wakati vita vya Ghaza vinaendelea na utawala wa Kizayuni umeshadidisha mauaji ya wanawake na watoto wa Palestina, mtazamo na mwelekeo wa wananchi wa Marekani kuhusuu Israel, Palestina na Hamas nao unaendelea kubadilika. Haya yamebainika katika chunguzi mpya za maoni zilizofanywa nchini Marekani.
-
Kushadidi mivutano ya kisiasa baina ya Ufaransa na utawala wa Kizayuni
Apr 23, 2025 02:08Utawala wa Israel umefuta viza za wabunge na maafisa 27 wa Ufaransa wa mrengo wa kushoto siku mbili kabla ya safari yao ya kuelekea Palestina inayokaliwa kwa mabavu iliyopewa jina bandia la Israel.
-
Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Muqawama: Kuitetea Ghaza ni jukumu la Waislamu wote
Apr 21, 2025 07:16Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama amesema, kuitetea na kuiunga mkono Ghaza ni jukumu la watu wote, na akatoa wito kwa mataifa ya Kiislamu na wanazuoni wa Kiislamu kuwasaidia ndugu zao wanaodhulumiwa huko Palestina na katika Ukanda wa Ghaza, wakati huu ambapo utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza jinai zake dhidi yao.
-
Iran: Utawala wa Kizayuni ndio kizuizi pekee kwa Asia Magharibi kuwa eneo lisilo na silaha za nyuklia
Apr 20, 2025 05:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Abbas Araghchi amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ndio kizuizi pekee kwa Asia Magharibi kuwa eneo lisilo na silaha za nyuklia, akionya kwamba utawala huo unaokalia ardhi kwa mabavu unachochea chuki dhidi ya Iran huku wenyewe ukiendeleza mauaji ya kimbari katika eneo hili.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Israel haina uthubutu wa kutushambulia
Apr 20, 2025 02:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "si Israel pekee ambayo haina uthubutu wa kutushambulia, lakini hata Marekani pia haikubali kubahatisha kujiingiza kwenye chokochoko hatari kama hiyo."
-
Taasisi ya Palestina: Siku ya mateka wa Palestina; nembo ya mapambano yao katika jela za Israel
Apr 18, 2025 02:40Ofisi ya Habari ya serikali katika Ukanda wa Gaza imetaja tarehe 17 Aprili liyoadhimishwa jana Alhamisi ambayo imepewa jina la Siku ya Mateka wa Palestina kuwa ni inakumbusha mateso, maumivu na masaibu wanayopitia zaidi ya mateka elfu kumi wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni.
-
Serikali ya Al-Jolani Syria kuanzisha uhusiano rasmi na Israel mwishoni mwa 2026
Apr 16, 2025 11:32Mwanadiplomasia mmoja wa Uingereza amefichua kuwa kiongozi wa kundi la wanamgambo la Hay-at Tahrir al-Sham HTS Abu Mohammed al-Jolani ameihakikishia Uingereza kwamba Syria "itaanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia" na utawala wa Kizayuni wa Israel, itautambua utawala huo, na kubadilishana nao mabalozi ifikapo mwisho wa mwaka ujao wa 2026.