Afisa mkuu wa Hezbollah nchini Lebanon: Muqawama hauwezi kusalimu amri
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i129942-afisa_mkuu_wa_hezbollah_nchini_lebanon_muqawama_hauwezi_kusalimu_amri
Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah huku akisisitiza kuwa, uamuzi wa serikali ya Lebanon wa kuupokonya silaha muqawama ni uamuzi usio wa kisheria wala halali amesema: Muqawama ni utamaduni na utambulisho usioweza kutokomezwa.
(last modified 2025-10-11T08:57:00+00:00 )
Aug 24, 2025 11:56 UTC
  • Afisa mkuu wa Hezbollah nchini Lebanon: Muqawama hauwezi kusalimu amri

Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah huku akisisitiza kuwa, uamuzi wa serikali ya Lebanon wa kuupokonya silaha muqawama ni uamuzi usio wa kisheria wala halali amesema: Muqawama ni utamaduni na utambulisho usioweza kutokomezwa.

Akifafanua suala hilo, Sheikh Ali Da'mush, Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah nchini Lebanon, alisema siku ya Ijumaa kwamba: 'Uamuzi usio sahihi uliotolewa na serikali ya Lebanon wa kupokonya silaha muqawama sio tu ni ukiukaji wa hati ya kitaifa, bali pia hauna akidi ya kitaifa na kiwango cha chini kabisa cha mantiki.' Sheikh Ali Da'mush amesisitiza: Itawezekana vipi nchi ambayo ardhi yake inakaliwa kwa mabavu na adui, ambayo watu wake wanashambuliwa kila siku, watu wanazuiwa kurejea katika vijiji vyao na majumbani mwao, na watoto wake ambao bado wanashikiliwa mateka na adui, serikali yake iamue kuipokonya moja ya nguzo muhimu za nguvu ya nchi, yaani Muqawama?