-
Kiongozi: Mataifa ya Kiislamu lazima yavunje uhusiano na Israel kukabiliana na 'jinai za maangamizi' inazofanya Ghaza
Sep 07, 2025 23:46Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema lazima mataifa ya dunia hususan nchi za Kiislamu zivunje uhusiano wote wa kibiashara na kisiasa na utawala wa kizayuni wa Israel ili kukabiliana na jinai zake za maangamizi unazofanya katika Ukanda wa Ghaza.
-
Araqchi: Nchi 3 za Ulaya lazima zibadili njia yao ya uharibifu
Sep 07, 2025 08:31Katika makala yake kwenye gazeti la The Guardian, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kwamba nchi tatu za Ulaya (Ufaransa, Uingereza na Ujerumani), zinapaswa kubadili mkondo wao wa uharibifu, akisisitiza kuwa: "Mchezo huu hautakuwa na matokeo yanayotarajiwa kwa nchi hizo, bali utakuwa na matokeo kinyume na utasababisha kutengwa zaidi kwa nchi hizo tatu kwa kuziondoa katika diplomasia ya baadaye."
-
Mkuu wa Majeshi ya Iran: Marekani, Israel zilishindwa kudhoofisha uwezo wa Iran wa nyuklia, makombora na ulinzi wa anga
Sep 07, 2025 03:07Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Amir Hatami, amesema Marekani na utawala wa Israel zililenga kudhoofisha uwezo wa nyuklia, makombora na ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu wakati wa vita vya siku 12 mwezi Juni mwaka huu, lakini walishindwa kufikia malengo yao makuu.
-
Araghchi: Iran na IAEA zinakaribia kuunda fremu mpya ya ushirikiano
Sep 06, 2025 23:20Iran imesema imekaribia sana kubuni mfumo mpya wa ushirikiano baina yake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), miezi kadhaa baada ya mashambulizi ya anga ya Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi hii kuipelekea Tehran kusimamisha ushirikiano wake na taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa.
-
Sambamba na kuanza duru mpya ya mazungumzo, Iran yatilia mkazo diplomasia katika kadhia ya nyuklia
Sep 06, 2025 03:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa liidhinishe juhudi za kidiplomasia katika kushughulikia mpango wa nyuklia wa Tehran na kukomesha vitendo vya "kinyume na sheria" vya Ulaya.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Sutafahamu zilizotokea baina yetu na Qatar zimeondolewa
Sep 05, 2025 23:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Abbas Araghchi amesema, mazungumzo yake na viongozi wa Qatar yalikuwa yenye faida na mafanikio makubwa na yalifanyika kwa uzito maalumu na akaongezea kwa kusema: "kwa bahati nzuri, hakuna tofauti zozote kati ya nchi hizi mbili, na sutafahamu iliyojitokeza imetatuliwa kikamilifu na ziara hii".
-
"Hatua ya nchi za Ulaya kuamilisha utaratibu wa snapback ni ya kiholela"
Sep 05, 2025 08:38Khatibu wa Muda wa Swala ya Ijumaa iliyoswalia leo hapa Tehran amesema: Kwa mujibu wa taarifa ya mwisho ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, jaribio lolote la kubadilisha Azimio Nambari 2231 linadhoofisha itibari ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kwamba hatua ya nchi tatu za Ulaya ya kuamilisha utaratibu wa "snapback" wa kurejesha vikwazo vya baraza hilo dhidi ya Iran ni ya kiholela.
-
IRGC: Adui hana ubavu wa kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran
Sep 05, 2025 07:33Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema Israel na washirika wake hawana uwezo wala ubavu wa kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran, hivyo basi, wamekimbilia operesheni za vita vya kisaikolojia.
-
Iran yaitaka dunia ilaani mashambulizi dhidi ya vituo vyake vya nyuklia
Sep 05, 2025 07:32Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Iran amesema Marekani na utawala wa Israel zilifanya mashambulizi ya kimakusudi dhidi ya vituo vya nyuklia ya Iran, licha ya vituo hivyo kuwa chini ya usimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Nyuklia.
-
Araqchi: 'Iran itaendelea kuunga mkono Muqawama wa Palestina dhidi ya Israel'
Sep 05, 2025 03:37Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesisitiza dhamira ya nchi hiyo ya kuunga mkono Muqawama halali na mapambano ya watu wa Palestina dhidi ya utawala vamizi wa Israel hadi pale haki zao zitakaporejeshwa kikamilifu.