-
Baghaei: Marekani ni tishio kubwa zaidi kwa amani na usalama wa kimataifa
Dec 01, 2025 06:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya iran amesema kuhusu vitendo vya Marekani dhidi ya amani ya dunia kuwa, ukweli ni kwamba Marekani ni tishio kubwa zaidi kwa amani na usalama wa kimataifa, na hivi sasa tunashuhudia matumizi maovu ya nguvu za Marekani katika nchi kama Venezuela na Afrika Kusini.
-
Katika mazungumzo na Fidan, Rais wa Iran aziasa nchi za Kiislamu zisahilishe badala ya kutatiza mambo
Dec 01, 2025 03:01Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hali hasasi na nyeti iliyopo hivi sasa katika Ulimwengu wa Kiislamu na kueleza kwamba: "wakati maadui wa pamoja wa mataifa ya Kiislamu wanatafuta njia za kuzidisha mashinikizo, ingetarajiwa nchi za Kiislamu zirahisishiane hali na mazingira na kujiepusha na utatizaji wa mambo".
-
Uvumbuzi wa Bioteknolojia Iran: Manyoya ya kuku kuwa lishe ya mifugo
Nov 30, 2025 23:20Iran imezindua uvumbuzi wa kisayansi unaoweza kubadilisha tasnia ya mifugo na kuku, kuimarisha usalama wa chakula wa ndani na kupunguza utegemezi wa uagizaji wa chakula cha mifugo kutoka nje.
-
Kituo kipya cha Treni cha Maria Mtakatifu chafunguliwa Tehran
Nov 30, 2025 23:19Halmashauri ya Jiji la Tehran imezindua rasmi kituo kipya cha metro (treni ya chini ya ardhi) kinachoitwa Maryam-e Moqaddas , yaani Maria Mtakatifu , kama ishara ya kuonyesha maelewano na kuishi kwa amani baina ya dini mbalimbali nchini humo.
-
Qalibaf: Hatua ya Australia dhidi ya Iran haitaweza kuzuia ushawishi wa IRGC
Nov 30, 2025 09:04Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge la Iran) Mohammad Baqer Qalibaf amelaani vikali hatua ya serikali ya Australia ya kuliweka katika orodha nyeusi Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), akibainisha kuwa hatua hiyo haitaweza kuzuia ushawishi wa IRGC.
-
Biashara ya nje ya Iran yapindukia dola bilioni 76.5 kuanzia Machi hadi Novemba
Nov 30, 2025 08:45Biashara ya nje ya Iran katika miezi minane ya kwanza ya mwaka huu kwa mujibu wa kalenda ya Iran ya Hijria Shamsia yaani (Kuanzia Machi 21, 2025 hadi Novemba 21 mwaka huu) imefikia tani milioni 131.054, yenye thamani ya dola bilioni 76.537.
-
Barua ya Pezeshkian kwa Umoja wa Mataifa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Palestina
Nov 30, 2025 04:12Katika ujumbe wake kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Palestina ya tarehe 29 Novemba, Rais wa Iran ametangaza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalichukulia suluhu pekee la kikanuni la kadhia ya Palestina kuwa ni kukomesha uvamizi wa kupangwa wa ardhi ya kihistoria ya watu wa Palestina, kurejea wakimbizi wa Kipalestina, na kutekeleza haki yao ya kujitawala.
-
Kwa mnasaba wa Siku ya Mshikamano, Iran yasema: Palestina ni jeraha kubwa zaidi linaloungulisha dhamiri ya wanadamu
Nov 29, 2025 23:49Kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesisitizia tena uungaji mkono usioyumba wa Jamhuri ya Kiislamu kwa wananchi madhulumu wa Palestina, ikiielezea hali yao kama "jeraha kubwa zaidi linaloungulisha dhamiri ya wanadamu."
-
Mkuu wa Jeshi: Iran iko tayari kutoa jibu kali kwa vitisho vya popote pale
Nov 29, 2025 09:43Kamanda Mkuu wa Jeshi amesema, Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeshajiweka tayari kikamilifu kutoa jibu kali kwa tishio lolote dhidi ya maslahi yake ya taifa, na kusisitiza kwamba mkakati wa ulinzi wa Iran umejengwa juu ya msingi wa kuzuia hujuma.
-
Wanafunzi wa Iran wang'ara katika Mashindano ya Hisabati ya Marekani
Nov 29, 2025 03:40Wanafunzi wa Iran washinda dhahabu na fedha katika Mashindano ya Hisabati ya Marekani (AMO) ya mwaka huu wa 2025.