-
Waziri wa Ulinzi: Iran imejipanga kutoa majibu makali zaidi ikishambuliwa kijeshi
Nov 28, 2025 23:57Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ipo katika kiwango cha juu zaidi cha utayari wa kijeshi kuwahi kushuhudiwa, akisisitiza kuwa kila kitendo cha uhasama kitapokewa kwa majibu “makali na mazito kuliko wakati wowote uliopita.”
-
Iran yasusia droo ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 kufuatia kukataliwa viza na Marekani
Nov 28, 2025 23:18Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (FFIRI) limetangaza kuwa halitohudhuria droo ya Kombe la Dunia FIFA 2026 wiki ijayo mjini Washington, baada ya Marekani kukataa kutoa viza kwa baadhi ya wajumbe wa msafara wao.
-
Iran yalaani jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan
Nov 28, 2025 08:15Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imelaani vikali jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na mauaji na mateso ya wakaazi wa eneo hilo.
-
Araghchi: Mazungumzo maana yake ni mazungumzo, si ukidteta; Marekani ijirekebishe kwanza
Nov 28, 2025 03:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Tehran itaendelea kuwa muwazi kuhusu mazungumzo, na msimamo wake utaendelea kuwa ule ule kwamba mazungumzo maana yake ni mazungumzo, si udikteta. Inaweza kufikiria kufanya mazungumzo na Marekani, lakini tu ikiwa Washington itabadilika na kuacha madai yake yasiyo na mantiki. Iingie kwenye mazungumzo ya kuheshimiana na ya usawa si ya kufanyiana udikteta.
-
Mwakilishi wa Iran akosoa undumilakuwili wa UN
Nov 28, 2025 03:03Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na jamii za wachache amekosoa misimamo ya nyuso mbili na ya kindulimakuwili la Umoja wa Mataifa katika kuyaendea masuala mbalimbali duniani ambayo yanapingwa na madola ya kibeberu.
-
Silaha za mauaji ya halaiki na sera za undumilakuwili za Washington na Tel Aviv, chanzo cha migogoro ya kiusalama Magharibi ya Asia
Nov 28, 2025 02:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesema, yanayoendelea kujiri katika eneo la Magharibi ya Asia ambayo ni vita vya kudumu, uchokozi wa kivamizi, mauaji ya kimbari na kujipanua kikoloni utawala wa kizayuni wa Israel, ni matokeo ya moja kwa moja ya uungaji mkono wa Marekani na uridhishaji unaofanywa na baadhi ya nchi za Ulaya kwa utawala huo haramu.
-
Kiongozi Muadhamu: Marekani haina hadhi ya kuwa na uhusiano na Iran
Nov 27, 2025 23:30Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kwenye hotuba yake kupitia televisheni ya taifa kwamba, Marekani haina hadhi ya kuwa na mahusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na Marekani na Israel ni vita vilivyopangwa kwa muda wa miaka 20 lakini taifa la Iran limeshinda na adui ameshindwa.
-
Larijani: Kuunga mkono umoja wa Umma wa Kiislamu ni mojawapo ya vipaumbele vikuu vya Iran
Nov 27, 2025 23:29Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa kulinda na kutetea umoja wa Umma wa Kiislamu ni miongoni mwa vipaumbele vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Jeshi la Wanamaji la Iran kuzindia zana mpya za kivita
Nov 27, 2025 23:16Admeri Shahram Irani, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran, ametangaza mipango ya kuzindua vifaa vipya na kuunganisha meli mpya katika jeshi hilo.
-
Larijani: Vita vya siku 12 ni matokeo ya njama za miaka mingi za Marekani na Wazayuni
Nov 27, 2025 02:30Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesisitiza katika mkutano na wasomi wa Pakistan kwamba vita vya siku 12 ilivyolazimishwa Iran kupigana ni matokeo ya njama kubwa za Marekani na utawala wa Kizayuni na vilipangwa miaka mingi nyuma.