-
Mipango na malengo makubwa ya Iran kwa ajili ya kushirikiana na nchi za Kiafrika
Apr 21, 2025 05:41Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeratibu mipango na kuainisha malengo yake kwa ajili ya ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi na bara la Afrika.
-
Araghchi: Wamarekani hawakuzungumzia suala jengine ghairi ya kadhia ya nyuklia
Apr 21, 2025 03:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuhusu mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana yanayofanyika kati ya Iran na Marekani kwa kusema: "mazungumzo yetu yanahusu masuala ya nyuklia na hatutakubali maudhui nyingine yoyote".
-
IRGC kuzindua manowari mpya kama za US, au bora zaidi
Apr 20, 2025 22:55Kamanda wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Admeli Alireza Tangsiri amesema yumkini SEPAH ikazindua manowari mpya ambazo muundo wake unashabihiana au utakuwa bora zaidi kuliko wa Marekani.
-
Tathmini ya duru ya pili ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani mjini Roma
Apr 20, 2025 09:41Duru ya pili ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya timu ya mazungumzo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ujumbe wa Marekani ilifanyika Jumamosi ya jana Aprili 19, huko Roma, mji mkuu wa Italia.
-
Mwanadiplomasia wa zamani wa Iran: Mazungumzo na Marekani yanaendelea vizuri
Apr 20, 2025 09:19Msemaji wa zamani wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran na balozi wa zamani wa Iran nchini Italia amesema: "Mazungumzo na Marekani yamekuwa na mwanzo mzuri kimuundo na kiujuma.
-
Araghchi: Mazungumzo ya kiufundi kati ya Iran na Marekani yataanza Jumatano nchini Oman
Apr 20, 2025 02:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi ameashiria kumalizika kwa duru ya pili ya mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana ya nyuklia kati ya Iran na Marekani yaliyofanyika jana Jumamosi mjini Rome, Italia na kueleza kwamba, mazungumzo ya kiufundi katika ngazi ya wataalamu yataanza siku ya Jumatano nchini Oman.
-
Iran: Utawala wa Kizayuni ndio kizuizi pekee kwa Asia Magharibi kuwa eneo lisilo na silaha za nyuklia
Apr 20, 2025 02:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Abbas Araghchi amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ndio kizuizi pekee kwa Asia Magharibi kuwa eneo lisilo na silaha za nyuklia, akionya kwamba utawala huo unaokalia ardhi kwa mabavu unachochea chuki dhidi ya Iran huku wenyewe ukiendeleza mauaji ya kimbari katika eneo hili.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Israel haina uthubutu wa kutushambulia
Apr 19, 2025 23:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "si Israel pekee ambayo haina uthubutu wa kutushambulia, lakini hata Marekani pia haikubali kubahatisha kujiingiza kwenye chokochoko hatari kama hiyo."
-
Press TV: Duru ya pili ya mazungumzo ya Iran na Marekani imefanyika Rome katika 'anga chanya'
Apr 19, 2025 11:02Duru ya pili ya mazungumzo ya nyuklia yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani imefanyika katika mji mkuu wa Italia, Rome leo Jumamosi katika "anga chanya". Hayo yameelezwa na ripota wa chaneli ya televisheni ya Press TV.
-
Mwito wa Iran kwa jamii ya kimataifa wa kuzingatiwa hali ya Gaza
Apr 19, 2025 10:46Esmail Baghaei, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuzingatia kwa uzito jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Gaza.