Matokeo ya Mkutano wa Istanbul kati ya Iran na Troika ya Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i128788-matokeo_ya_mkutano_wa_istanbul_kati_ya_iran_na_troika_ya_ulaya
Suala la kuondoa vikwazo na kutilia mkazo haki ya Iran ya kurutubisha urani ni miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika ajenda ya "Mkutano wa Istanbul." Pande hizo zimesisitiza udharura wa kuendeleza mazungumzo.
(last modified 2025-07-26T09:10:06+00:00 )
Jul 26, 2025 09:10 UTC
  • Matokeo ya Mkutano wa Istanbul kati ya Iran na Troika ya Ulaya

Suala la kuondoa vikwazo na kutilia mkazo haki ya Iran ya kurutubisha urani ni miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika ajenda ya "Mkutano wa Istanbul." Pande hizo zimesisitiza udharura wa kuendeleza mazungumzo.

Majid Takht -Ravanchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisiasa ameshiria baada ya mazungumzo ya jana Ijumaa huko Istanbu kati ya Iran na Troika ya Ulaya yaani (Ujerumani, Ufaransa na Uingereza) kwamba mkutano huo ni muendelezo wa majadiliano ya huko nyuma kuhusu kadhia ya nyuklia ambayo hufanyika mara kwa mara na akasema: Tumeeleza upinzani wetu kwa mijadala inayohusiana na utaratibu wa Snapback. 

Takht-Ravachi ameongeza kuwa: Waziri wa Mambo ya Nje hivi karibuni alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kumweleza misimamo yetu ya kisheria kuhusu suala hilo, na kusema: Nchi hizo haziwezi kutumia utaratibu wa "Snapback." Tulitoa maoni yetu kwa uwazi na barua hiyo imesajiliwa katika Umoja wa Mataifa na kukabidhiwa kwa wanachama wa Baraza la Usalama. Aidha tulizungumzia haki zetu katika fremu ya mkataba wa NPT likiwemo suala la kurutubisha madini ya urani na kwamba urutubishaji ni miongoni mwa haki zetu na unapasa kuendelea kufanyika ndani ya Iran. Mjadala wa kuondolewa vikwazo na ukweli kwamba vikwazo vya kidhalimu dhidi ya Iran viondolewe haraka iwezekanavyo ilikuwa mada nyingine tuliyozungumzia katika mkutano wa jana mjini Istanbul, Uturuki. 

Takht- Ravanchi 

Kazem Gharib Abadi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisheria na Kimataifa pia alisema baada ya kumalizika mkutano wa Istanbul kwamba tehran na Troika ya Ulaya zimekubaliana kuendeleza mashauriano ambapo. Vilevile  ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa X kwamba: "Dakta Takht-Ravanchi na Mimi, tumekuwa mazungumzo ya kina na ya wazi na maafisa wa kisiasa wa nchi tatu za Ulaya na Umoja wa Ulaya. Hatua zilizopigwa karibuni kuhusu kuondoa vikwazo na kadhia ya nyuklia zimejadiliwa na kuchunguzwa. Aidha tumekosoa vikali misimamo yao kuhusu vita vya kichokozi vya karibuni dhidi ya taifa letu, na tumewaeleza waziwazi misimamo yetu ikiwa ni pamoja na kuhusiana na utaribu unaojulikana kama Snapback. 

Hii ni katika hali ambayo Troika ya Ulaya imewasilisha riwaya nyingine kuhusu matokeo ya Mkutano wa Istanbul. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani imetangaza katika taarifa yake kuwa Troika ya Ulaya imewasilisha pendekezo la masharti kwa Iran katika Mkutano wa Istanbul kuhusu kuongeza muhula wa kuhuisha utaratibu wa Snapback. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani imetangaza kuwa: Troika ya Ulaya iko tayari kuhuisha mfumo wa Snapback; hata hivyo tumependekeza kwa sharti kuwa Iran itekeleze majukumu yake ya kisheria na kuheshimu vigezo maalumu. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujeumani hata hivyo haikutoa maelezo kuhusu majukumu hayo ya kisheria na vigezo maalumu, lakini Iran kwa upande wake imesisitiza kuwa ilizingatia na kutekeleza majumukumu yake ya kinyuklia. Berlin imesema mwishoni mwa taarifa yake kuwa: Tunaitaka Iran ichague njia ya diplomasia. 

Kabla ya hapo, nchi za Ulaya zilianisha mwishoni mwa mwezi Agosti kuwa muhula wa kuhuisha mfumo huo. Hata hivyo vyombo vya habari vya Magharibi vimeripoti kuwa kuna uwezekano utaratibu huo ukarefushwa kwa muda kwa miezi sita. Shirika la habari la Reuters liliandika kabla ya Mkutano wa Istanbul likiwanukuu wanadiplomasia watatu wa Ulaya, mwanadilpmasia wa kikanda na wa Kiirani kwamba: Ajenda kuu ya Mkutano wa Istanbul itahusu utaratibu wa Snapback. Walisema kuwa nchi za Ulaya zina mpango wa kutoa pendekezo la kuongeza muda wa miezi sita wa kuhuisha utaratibu huo. 

Mkabala wake, Iran inapasa iwajibike kuhusu masuala muhimu ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo na Washington, ushirikiano kamili na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) na kutoa majibu kuhusu akiba yake ya urani iliyorutubishwa kwa kiwango kikubwa. 

Iran kwa upande wake inaamini kuwa, kujikita katika utaratibu wa kurejesha vikwazo ni kinyume cha sheria na kutangaza kuwa: Itajibu hatua yoyote ya nchi za Ulaya katika uwanja huo. Kadhalika, madai ya nchi za Ulaya kwamba upo ulazima kwa Iran kurejea kwenye meza ya mazungumzo yameibuliwa huku Tehran siku zote ikichagua njia ya diplomasia, lakini ni Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ndizo zilizoishambulia Iran huku mazungumzo yakiendelea. Nchi za Ulaya, ikiwemo Ujerumani, pia zilifadhilisha kuunga mkono vitendo hivyo vya uvamizi huku nyingine zikinyamaza kimya. 

Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuhusu vitisho vya Troika ya Ulaya kwamba nchi hizo tatu haziwezi na hazipaswi kuruhusiwa kuhoji hadhi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kutumia vibaya azimio ambalo wao wenyewe wamelipuuza.

Sayyid Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran