-
Iran na China ni ngome isiyoweza kupenywa na vikwazo vya Marekani
Apr 17, 2025 02:13Wizara ya Fedha ya Marekani imezidisha mashinikizo dhidi ya Tehran kwa kukiwekea vikwazo kiwanda cha kusafisha mafuta cha China kwa madai ya kununua mafuta ya Iran. Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kuwa si tu vikwazo hivyo havijazuia mauzo ya mafuta ya Iran, bali pia vimezidisha ushirikiano wa kiuchumi na kijiografia kati ya Iran na China.
-
Gharibabadi: Iran haina haja ya kupoteza muda kwenye mazungumzo
Apr 17, 2025 02:12Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayehusika na Sheria na Masuala ya Kimataifa amesema kuwa duru ijayo ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani itafanyika kama ilivyopangwa na kwamba Tehran haina haja ya kupoteza muda.
-
Baghaei: Misimamo inayogongana ya Marekani ni ishara ya kutokuwa na nia njema na ya dhati katika mazungumzo
Apr 17, 2025 00:00Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Esmail Baghei ametoa mjibizo kwa msimamo wenye mgongano ulioonyeshwa na Steve Witkoff, mjumbe maalumu wa Rais wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati na mwakilishi wa nchi hiyo katika mazungumzo na Iran.
-
Iran: Urutubishaji urani 'haujadiliki', mazungumzo chini ya mashinikizo hayatakuwa na tija
Apr 16, 2025 08:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema urutubishaji wa madini ya urani ukiwa ni sehemu ya mpango wa amani wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu "haujadiliki" na kwamba mazungumzo ya Tehran na Washington hayatazaa matunda ikiwa yatafanyika kwa mashinikizo na bila ya pande mbil kuheshimiana.
-
Taratibu ambazo Iran inaona zinahitajika ili kurekebisha Mkataba wa Umoja wa Mataifa
Apr 16, 2025 06:19Kazem Gharibabadi, Naibu Waziri wa Masuala ya Kisheria na Masuala ya Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amewasilisha mapendekezo ya Jamhuri ya Kiislamu kwa wajumbe wa Kundi la Marafiki wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa katika kikao cha tatu cha Waratibu wa Kitaifa wa Hati ya Marafiki wa Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na Moscow.
-
IRGC: Usalama wa taifa na uwezo wa kijeshi wa Iran ni 'mistari myekundu, haijadiliki'
Apr 15, 2025 23:45Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesisitiza kuwa, usalama wa taifa na uwezo wa kijeshi wa Iran hauwezi kujadiliwa kwa namna yoyote ile.
-
Kuimarishwa biashara kati ya Iran na Eurasia; hatua ya kimkakati
Apr 15, 2025 11:14Biashara kati ya Iran na Umoja wa Kiuchumi wa Nchi za Eurasia imekuwa ikistawi siku hadi siku licha ya vikwazo vikubwa vya kiuchumi vilivyowekwa na Magharibi dhidi ya Iran. Kwa mujibu wa tawimu mpya zilizotolewa hivi karibuni, uuzaji bidhaa za Iran kwa nchi wanachama wa umoja huo katika mwaka uliopita uliongezeka kwa asilimia 20 na kufikia karibu dola bilioni mbili.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Hatufurutu mpaka katika kuyatazama mazungumzo ya Oman kwa jicho zuri au baya
Apr 15, 2025 09:40Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, ufuatiliaji ndicho kiungo kinachokosekana katika kufanikisha malengo ya nchi na akasisitiza kuwa ajenda ya pamoja ya mihimili mitatu ya dola ni kufanya jitihada za kufanikisha kaulimbiu ya mwaka huu.
-
Iran itawapokea wanafunzi na wasomi kutoka vyuo vikuu vya Gaza
Apr 15, 2025 06:46Iran itawapokea kwa mikono miwili wasomi na wanafunzi wa Kipalestina katika vyuo vikuu vya Iran kufuatia uharibifu mkubwa wa taasisi za elimu katika Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi ya utawala haramu wa Israel.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudia wajadili mazungumzo ya Oman
Apr 15, 2025 04:36Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudi Arabia wamefanya mazungumzo ya simu na kujadiliana kuhusu uhusiano wa pande mbili na maendeleo ya kikanda na kimataifa.