-
Iravani: Tuhuma zisizo na msingi za US zinazidi kudhihirisha sera zake za kiuadui dhidi ya Iran
Mar 22, 2025 08:17Amir Saeed Iravani, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amekanusha tuhuma zisizo na msingi za Marekani dhidi ya Iran na akasema: "tuhuma hizi zisizo na msingi kwa mara nyingine tena zinazidi kudhihirisha sera za uadui za serikali ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran".
-
Kofi kali; Jibu la taifa la Iran kwa uhabithi wa Marekani
Mar 22, 2025 03:15Akizungumza jana Ijumaa katika kikao na maelfu ya watu wa matabaka tofauti katika siku ya kwanza ya mwaka wa Kiirani wa 1404 Hijria Shamsia, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiogopi vitisho vya Marekani, na kwamba iwapo italisababishia madhara yoyote taifa la Iran, itapata kipigo na kofi kali.
-
Mwangwi wa matamshi ya Imam Khamenei katika vyombo vya habari duniani
Mar 22, 2025 01:06Matamshi yaliyotolewa jana na Kiongozi Muadhamu wa mapinduzi ya Kislamu, Imam Ali Khamenei katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Hijria Shamsia akijibu vitisho vya Rais wa Marekani, Donald Trump, yameakisiwa kwa mapana na marefu katika vyombo vya habari vya kimataifa.
-
Imam Khamenei: Iwapo Wamarekani watafanya uhabithi kwa taifa la Iran, watazabwa kofi kali
Mar 21, 2025 11:13Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameionya Marekani dhidi ya kutumia lugha ya vitisho dhidi ya Iran.
-
Ayatullah Seddiqi: Uwekezaji kwa ajili ya uzalishaji utastawisha nchi
Mar 21, 2025 09:37Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameeleza kuwa, uzalishaji ni mhimili wa ustawi wa maisha ya watu na ni chachu ya maendeleo na ajira na kusema: "Serikali lazima irahisishe njia za kuvutia viitegauchumi na rasilimali za wananchi kwa kutumia wataalamu mahiri."
-
Mkuu wa ujasusi Israel akiri Iran "imejipenyeza kwa kina", amlaumu Netanyahu
Mar 21, 2025 04:09Kiongozi wa shirika la ujasusi wa ndani la utawala wa Israeli amesema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ndiye anayepaswa kulaumiwa kutokana na matatizo makubwa ya utawala huo, ikiwemo usimamizi mbovu uliosababisha kile alichotaja kuwa "upenyaji wa kina" wa Iran kwenye taasisi za kiusalama na kijasusi za Israel.
-
Kuakisiwa ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika vyombo vya habari vya kimataifa; Umma wa Kiislamu usimame dhidi ya jinai za Wazayuni
Mar 21, 2025 04:00Ujumbe wa Nowruz wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hususan matamshi yake kuhusiana na Ukanda wa Gaza, Lebanon, kadhia ya Palestina na Yemen umeangaziwa pakubwa na vyombo vya habari vya kimataifa vikiwemo vyombo vya habari vya eneo hili.
-
Waziri wa Mambo ya Nje: Iran itajibu barua ya Trump
Mar 20, 2025 23:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kwamba Jamhuri ya Kiislamu itajibu barua ya Rais wa Marekani Donald Trump katika siku zijazo kupitia njia zinazofaa.
-
Salamu za Nouruzi za Rais Pezeshkian kwa Wairan: Tutaifanya qadar yetu iwe bora na tukufu zaidi
Mar 20, 2025 09:18Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza katika ujumbe na salamu zake za Nouruzi kwa wananchi wa Iran kwamba, Nouruzi na Usiku wa Qadar (Lailatul-Qadr) ni miale miwili ya nuru moja na madhihirisho mawili ya hakika na ukweli mmoja, na akafafanua kwa kusema: "katika mzunguko mpya wa masiku, tutaifanya qadari yetu iwe bora na tukufu zaidi kuliko ilivyo sasa".
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Mwaka 1404 ni "Mwaka wa Uwekezaji kwa ajili ya Uzalishaji"
Mar 20, 2025 07:42Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu uwa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1404 hijria shamsia na kuutaja mwaka huu mpya kuwa ni "Mwaka wa Uwekezaji kwa ajili ya Uzalishaji."