-
Rais Pezeshkian: Wazayuni wakithubutu kufanya kosa, watapata jibu kali zaidi la Iran
Oct 02, 2024 10:02Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba operesheni ya makombora ya jana ya kujivunia ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya Israel kwa mara nyingine tena imethibitisha kwamba ngao ya chuma inayodaiwa Wazayuni ni dhaifu kuliko kioo.
-
Spika wa Bunge: Tumewaonyesha wavamizi sehemu ndogo tu ya uwezo wa Iran
Oct 02, 2024 09:27Mohammad Baqir Qalibaf, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza operesheni ya makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH dhidi ya utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa, wavamizi wameonyeshwa sehemu ndogo tu nguvu ya Iran.
-
Operesheni ya Ahadi ya Kweli-2: Hatua ya Iran ya kujilinda kihalali
Oct 02, 2024 08:47Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelitaja shambulio kali la makombora la Iran la Oktoba Mosi dhidi ya utawala haramu wa Israel kuwa ni haki yake halali ya kujilinda kwa msingi wa Kifungu cha 51 cha Hati ya Umoja wa Mataifa.
-
Araghchi: Tumejiandaa kwa mashambulio tarajio ya Israel, jibu letu litakalofuata litakuwa kali zaidi
Oct 02, 2024 08:46Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa, operesheni ya makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) dhidi ya maeneo ya utawala wa Kizayuni wa Israel yalikuwa ni ya kujihami kikamilifu na kusisitiza kuwa: Iwapo utawala wa Kizayuni utataka kujibu mashambulio hayo, basi jibu letu litakalofuata litakuwa kali zaidi.
-
Wakazi wa Tehran wakusanyika kuunga mkono mashambulio ya makombora dhidi ya Israel
Oct 02, 2024 08:44Wananchi wa mji mkuu wa Iran Tehran leo wamekusanyika katika medani ya Imam Hussein (as) na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa Operesheni ya Ahadi ya Kweli-2 ya mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya utawala haramu wa Israel.
-
Tathmini ya vipengele vya kijeshi vya Operesheni ya Ahadi ya Kweli -2: Jibu kwa shari za Israeli
Oct 02, 2024 07:44Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) jana usiku lilitoa taarifa likitangaza kuwa limeshambulia kitovu cha maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina (Israel) ikiwa ni katika kujibu mauaji ya shahidi Ismail Haniyeh, Sayyid Hassan Nasrullah na Meja Jenerali Abbas Nilforoushan Kamanda na mshauri wa ngazi ya juu wa IRGC huko Lebanon.
-
Ayatullah Khamenei: Njia pekee ya kumaliza vita Asia Magharibi ni kupungua uovu wa Marekani
Oct 02, 2024 07:23Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, chimbuko la matatizo ya eneo la Asia Magharibi ni mataifa kama Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zinazodai kwa uwongo kwamba, zinataka amani na utulivu.
-
Video na Picha zinazohusiana na mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel
Oct 02, 2024 06:44Shambulio halali kisheria la makombora lililofanywa na Iran kwa kulenga maeneo ya kijeshi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, na ambalo limetekelezwa kutokana na kuuawa shahidi viongozi wa Muqawama, limeibua wimbi kubwa la furaha na matumaini kwa wananchi wa eneo la Magharibi mwa Asia. Hapa chini tumeweka picha na video zinazohusiana na shambulio hilo lililopewa jina la Ahadi ya Kweli (2).
-
Iran yauandikia barua muhimu Umoja wa Mataifa na kutoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Oct 02, 2024 05:37Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua Katibu Mkuu na Rais wa Baraza la Usalama la umoja huo kufuatia operesheni ya makombora iliyofanywa na Iran, na kusisitiza kuwa, endapo utawala wa Israel utarudia tena vitendo vyake vinavyokiuka sheria za kimataifa, jibu litakalotolewa tena na Iran litakuwa la haraka, madhubiti na kali zaidi kuliko lililiotangulia.
-
Araghchi: Shambulio la Iran dhidi ya utawala wa Israel limetokana na haki ya uhalali wa kujilinda
Oct 02, 2024 04:39Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelitaja shambulio kali la makombora la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala katili wa Israel kuwa limeendana na haki ya halali wa kujilinda ya Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UN).