-
Iran yaboresha mfumo wa hali ya juu wa ulinzi
Sep 16, 2024 09:00Kamanda wa ngazi za juu katika Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIADF), ambacho ni tawi la Jeshi la Iran, ametangaza kuimarishwa mojawapo ya mifumo ya juu zaidi ya ulinzi katika kikosi hicho.
-
Kiongozi Muadhamu: Kuna udharura wa kulinda utambulisho wa Umma wa Kiislamu
Sep 16, 2024 08:49Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kulinda utambulisho wenye thamani wa Umma wa Kiislamu ni dharura na kuongeza kuwa: "Kadhia ya 'Umma wa Kiislamu" haipaswi kusahaulika hata kidongo.
-
Ubalozi wa Iran London kwa Wamagharibi: Zungumzeni na Iran kwa lugha ya heshima
Sep 16, 2024 03:18Ubalozi wa Iran mjini London huko Uingereza umezungumzia tukio la kurushwa angani kwa mafanikio satelaiti ya utafiti ya "Chamran-1" na maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu katika tasnia ya anga za juu licha ya vikwazo visivyo vya haki vya nchi za Magharibi na kusema: Zungumzeni na Iran kwa lugha ya heshima, na si kwa lugha ya vikwazo.
-
Rais Pezeshkian: Lengo kuu la Iran ni umoja, mshikamano na maelewano katika Umma wa Kiislamu
Sep 16, 2024 02:58Huku akielezea malengo ya safari yake ya siku tatu nchini Iraq, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian amesema kuwa: Lengo kuu la serikali ni umoja, mafungamano na maelewano katika Umma mzima wa Kiislamu.
-
Qalibaf: Madai ya uwongo ya nchi za Magharibi yanakwamisha mazungumzo yenye tija
Sep 15, 2024 23:23Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa hakutakuwepo mazungumzo yoyote yenye tija maadamu nchi za Ulaya na nyingine za Magharibi zinataka kuandaa mazingira kwa ajili ya mashinikizo zaidi kwa kutoa madai ya uwongo.
-
Bingwa wa kunyanyua vitu vizito wa Iran apeperusha bendera ya Palestina huko Finland
Sep 15, 2024 23:16Timu ya Iran ya kunyanyua vitu vizito imemaliza kibarua chake katika mashindano ya maveterani wa dunia kwa kupata medali moja ya dhahabu, mbili za fedha na mbili za shaba.
-
Safari ya Mohammad Eslam mjini Vienna inayolenga kubainisha pande tofauti za mpango wa amani wa nyuklia wa Iran
Sep 15, 2024 22:59Mohammad Eslami, Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekwenda Vienna Austria kushiriki katika mkutano mkuu wa mwaka wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA kwa lengo la kufafanua pande tofauti za mpango wa nyuklia wa Iran wenye malengo ya amani.
-
Safari ya kihistoria ya Rais Pezeshkian nchini Iraq, yenye matokeo chanya na ya wazi
Sep 15, 2024 07:03Safari ya siku tatu ya Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Iraq imemalizika katika hali ambayo matokeo ya safari hiyo yanaonekana kuwa chanya na ya wazi kabisa katika kuimarisha umoja na mshikamano wa mataifa mawili.
-
Qalibaf asisitizia umoja wa Waislamu katika kadhia ya Palestina
Sep 15, 2024 04:02Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesisitizia haja ya Waislamu kote duniani kuwa na umoja na mshikamano katika suala la Palestina.
-
Iran: Mafanikio yetu katika uga wa teknolojia ni pigo kwa maadui
Sep 15, 2024 03:59Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, hatua ya satelaiti ya utafiti ya Iran iliyopewa jina la "Chamran-1" kurushwa katika anga za mbali kwa mafanikio ni pigo kwa maadui wanaoliwekea taifa hili vikwazo visivyo na mantiki.