-
Iran: Mapigo tutakayojibu dhidi ya shambulio la Israel yataendana na sheria za kimataifa
Oct 29, 2024 04:30Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu inabaki nayo haki yake ya msingi ya kujibu mashambulio ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ardhi yake na kwamba ulipizaji kisasi utakaofanywa na Tehran utaendana kikamilifu na sheria za kimataifa.
-
Kikao cha tano cha Kamisheni ya Pamoja ya Iran na Tanzania kimeshirikisha wanawake wengi
Oct 29, 2024 04:25Makamu wa Rais wa Iran anayehusika na Masuala ya Wanawake na Familia ametangaza kuwa kikao cha tano cha Kamisheni ya pamoja ya Iran na Tanzania kimefanyika kwa kushirikisha wanawake wengi na kwa lengo la kupanua uhusiano wa kiuchumi, kibiashara, kijamii na kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili.
-
Nguvu za kijeshi za Iran hazijaathiriwa na shambulio la Israel
Oct 28, 2024 23:39Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran (SNSC) Ali Akbar Ahmadian amesema hujuma ya hivi karibuni za Israel haijapunguza hata kidogo nguvu za kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
X yasimamisha akaunti ya Ayatullah Khamenei ya lugha ya Kiebrania
Oct 28, 2024 23:38Mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter, umesimamisha akaunti ya lugha ya Kiebrania ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.
-
Iran imesharekebisha uharibifu mdogo uliosababishwa na mashambulizi ya Israel
Oct 28, 2024 23:31Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh anasema hujuma ya hivi majuzi wa utawala wa Israel dhidi ya vituo kadhaa vya kijeshi vya Iran ulisababisha uharibifu "mdogo" ambao ulirekebishwa mara moja.
-
Iran: Kiburi cha Israel kinatokana na uungaji mkono usio na kikomo wa Marekani
Oct 28, 2024 09:24Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, sababu kuu ya kiburi na ufidhuli wa utawala wa Kizayuni wa Israel ni uungaji mkono usio na kikomo wa Marekani.
-
Bangladesh yalaani uvamizi wa Israel dhidi ya Iran
Oct 28, 2024 08:56Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Bangladesh sawa na nchi nyingine nyingi za Kiislamu imelaani kitendo cha kichokozi cha utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.
-
Mifano ya makosa ya kimahesabu yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni kuhusu nguvu na uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Oct 28, 2024 06:17Akizungumza jana Jumapili mjini Tehran, na familia za Mashahidi wa Usalama, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umefanya makosa makubwa ya kimahesabu kuhusu Iran na kusisitiza kuwa utawala huo unapaswa kuadhibiwa na kufahamishwa nguvu, irada na ubunifu wa taifa la Iran na vijana wa nchi hii.
-
Rais Pezeshkian: Iran itatoa jibu linalostahiki kwa uchokozi wa Israel dhidi yake
Oct 28, 2024 03:25Rais Masoud Pezeshkian amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haipendi vita lakini iko imara katika kujihami na kulinda usalama wa wananchi wake na itatoa jibu linalostahiki kwa uchokozi wa utawala wa Kizayuni dhidi yake.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Misri wafanya mazungumzo kuhusu chokochoko mpya za Israel dhidi ya Iran
Oct 28, 2024 03:20Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri jana Jumapili ilitoa taarifa na kusema kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Badr Abdelatty amefanya mazungumzo ya simu na waziri mwenzake wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi na kujadiliana naye kuhusu shambulio la Israel la siku ya Jumamosi dhidi ya baadhi ya maeneo ya Iran.