-
Iran yakanusha madai ya Magharibi: Hatujaipatia Russia makombora yoyote ya balestiki
Sep 07, 2024 08:23Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekanusha madai kwamba inaipatia Russia makombora ya balestiki na kusisitiza kuwa madai hayo yanayotolewa na Marekani na washirika wake wa Magharibi ni ya upotoshaji na hayana msingi wowote.
-
Araghchi asisitiza kuimarishwa uhusiano wa Iran na Serbia
Sep 07, 2024 03:49Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesitiza umuhimu wa kutumia rasilimali zote zilizopo ili kuimarisha uhusiano kati ya Iran na Serbia, hasa katika sekta ya uchumi.
-
Iran: Adui anatiwa kiwewe na ustawi na maendeleo yetu ya nyuklia
Sep 06, 2024 23:42Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran amezungumzia maendeleo ya kupigiwa mfano iliyopata Jamhuri ya Kiislamu katika upande wa nishati ya nyuklia na kusema kuwa, licha ya kuweko vikwazo haramu vya Marekani dhidi yetu, lakini tumepiga hatua kubwa za maendeleo; na mabeberu wanatiwa kiwewe na ustawi wetu wa nyuklia.
-
Bahrain yataka kuimarisha uhusiano wake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Sep 06, 2024 23:18Bahrain imesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha uhusiano kati yake na Jamhurii ya Kiislamu ya Iran.
-
Maghala ya nyuklia ya Israel tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia
Sep 06, 2024 23:00Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni wa Israel ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa kikanda na wa ulimwengu mzima.
-
Sera ya kuunga mkono Palestina, kipaumbele cha serikali ya 14
Sep 06, 2024 09:13Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuunga mkono muqawama wa wananchi wa Palestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel ni moja ya vipaumbele vya serikali ya 14 na sehemu muhimu ya nguzo za siasa za nje za Iran.
-
Ayatullah Khatami: Israel inazidi kujiangamiza
Sep 06, 2024 07:30Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amegusia nasaha 13 za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kwa Serikali ya 14 ya Iran na kusema kuwa, mafanikio ya serikali hiyo yako chini ya kivuli cha kutekeleza kivitendo nasaha hizo za Kiongozi Muadhamu.
-
Iran yakanusha madai ya Marekani ya kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo
Sep 06, 2024 05:16Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekanusha madai ya Mwanasheria Mkuu wa Marekani aliyedai kuwa eti Tehran inangilia uchaguzi wa nchi hiyo na kusema kuwa, kwa mara nyingine tena, tunakanusha madai yanarudiwarudiwa ya eti tunaingilia uchaguzi wa Marekani.
-
IRGC: Visiwa vya Iran katika Ghuba ya Uajemi vimetayarishwa kijeshi
Sep 06, 2024 03:58Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji katika Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amekagua utayarifu wa kijeshi katika eneo muhimu la kistratijia la Nazaat katika Ghuba ya Uajemi. Eneo hilo lina visiwa vinne vya Tunb Kubwa, Tunb Ndogo, Abu Musa, na Sirri karibu na Mlango-Bahari wa Hormuz.
-
Iran yalaani hatua ya Marekani ya kuiba ndege ya Rais wa Venezuela
Sep 05, 2024 23:32Msemaji Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani hatua ya serikali ya Marekani kukamata ndege inayotumiwa na rais wa Venezuela.