Mwandishi wa Uingereza: Wairani wanafanyia maskhara shambulio dhaifu la Israel
(last modified Sun, 27 Oct 2024 09:47:15 GMT )
Oct 27, 2024 09:47 UTC
  • Mwandishi wa Uingereza: Wairani wanafanyia maskhara shambulio dhaifu la Israel

Mwandishi wa Uingereza ameutaja “uchokozi wa kimaonyesho” wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya Iran kuwa ni dhihaka kwa watu wa nchi hiyo.

Mwandishi wa Uingereza, Patrick Wintour ameandika katika makala iliyochapishwa katika gazeti la "Guardian" la London, kwamba kiwango dhaifu cha mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran kimewafanya Wairani walifanyie mzaha shambulizi hilo.

Wintour ameandika, ni haki ya watu wa Iran kuamua jinsi ya kukabiliana na shambulio hili.

Gazeti la "The Guardian" liliandika katika ripoti yake jana, wakati wa kuchunguza shambulizi la utawala wa Israel katika ardhi ya Iran, kwamba mfumo wa ulinzi wa anga wa Iran ulikuwa bora zaidi kuliko mfumo wa Iron Dome wa Israel.

Mepama Jumamosi ya jana, utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia vituo vya kijeshi vya mikoa ya Tehran, Khuzestan na Ilam ambapo mfumo jumuishi wa ulinzi wa anga wa Iran uliweza kukabiliana kwa mafanikio na uchokozi huo wa utawala ghasibu wa Israel.

Kwa mujibu wa tangazo la Idara ya Mahusiano ya Umma ya Kambi ya Ulinzi wa Anga ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, uharibifu mdogo tu umefanyika katika baadhi ya maeneo, na kwamba tukio hilo bado linachunguzwa.