-
Raisi: Kutoa ruhusa ya kuchoma moto Qur'ani ni ishara ya ujinga mamboleo
Jul 24, 2023 07:38Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kutoa leseni ya kuidhalilisha na kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu ni kinyume na madai ya uhuru wa kusema na ni kielelezo cha "ujinga mamboleo".
-
Abdollahian: Nchi za Kiislamu zichukue msimamo imara dhidi ya kuvunjiwa heshima Qur'ani
Jul 24, 2023 01:13Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko Sweden na Denmark, akisisitiza umuhimu wa kuchukuliwa msimamo thabiti wa nchi za Kiislamu katika kulaani na kuzuia vitendo hivyo.
-
Kan'ani: Kama kuchoma Kitabu ni uhuru wa kusema, basi zama za kiza ni enzi za dhahabu kwa Ulaya
Jul 23, 2023 10:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amegusia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Ulaya Magharibi za Sweden na Denmark na kusema kuwa, kama kuchoma moto Kitabu ni uhuru wa kujieleza, basi zama za kiza barani Ulaya zitakuwa ni zama za dhahabu katika uhuru wa wananchi wa bara hilo.
-
Iran yataka kufanyike kikao cha dharura cha OIC kujadili kuvunjiiwa heshima Qur'ani Tukufu
Jul 23, 2023 04:12Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito wa kuitishwa kikao cha dharura cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiiislamu (OIC) kwa ajili ya kujadili kiitendo cha kuvunjiwa heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani nchini Sweden na Denmark.
-
Rais wa Iran: Hatua ya serikali ya Sweden ya kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani haitoshi
Jul 23, 2023 00:12Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatua ya serikali ya Sweden ya kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani haitoshi kwa namna yoyote ile, bali serikali ya nchi hiyo inapaswa kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wa jinai hiyo.
-
Kiongozi Muadhamu: Aliyeivunjia heshima Qur'ani Tukufu Sweden akamatwe na kukabidhiwa kwa mahakama za nchi za Kiislamu
Jul 22, 2023 07:59Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kutovukiwa adabu matukufu ya Waislamu hasa Qur'ani Tukufu huko nchini Sweden ni tukio chungu na ni njama hatari sana akisisitiza kuwa, aliyefanya jinai hiyo lazima aadhibiwe, na maulamaa wote wa Kiislamu wanaafikiana katika hilo.
-
Iran na Iraq zalaani vikali kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Denmark
Jul 22, 2023 07:19Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Denmark.
-
Ghalibaf: Kuvunjiwa heshima itikadi za Waislamu duniani hakuwezi kuachwa hivi hivi
Jul 22, 2023 07:18Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameilaani vikali serikali ya Sweden kwa kuandaa mazingira ya kuvunjiwa heshima tena Qur'ani Tukufu mjini Stockholm na kusema kuwa, kuzivunjia heshima itikadi za Waislamu duniani kuna gharama zake na serikali ya Sweden ndiyo inayobeba lawama.
-
Rais wa Iran aamuru balozi mpya wa Uswidi asiruhusiwe kuingia Iran baada ya kuvunjiwa heshima Qur'ani
Jul 22, 2023 04:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema kuwa, Iran haitamkubali balozi mpya wa Uswidi kufuatia kuvunjiwa tena heshima Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo ya Skandinavia, ambalo ni tukio la pili la aina hiyo katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja.
-
Iran yatoa wito kwa Uswidi iwaadhibu wale waliyoivunjia heshima Qur'ani Tukufu
Jul 22, 2023 00:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameitaka Uswidi kuwaadhibu wale waliohusika katika kitendo kiovu cha kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo ya Skandinavia, huku akiionya kuhusu "maamuzi madhubuti" ya nchi za Kiislamu iwapo jambo hilo halitashughulikiwa.