-
Iran yatoa wito kwa Uswidi iwaadhibu wale waliyoivunjia heshima Qur'ani Tukufu
Jul 22, 2023 00:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameitaka Uswidi kuwaadhibu wale waliohusika katika kitendo kiovu cha kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo ya Skandinavia, huku akiionya kuhusu "maamuzi madhubuti" ya nchi za Kiislamu iwapo jambo hilo halitashughulikiwa.
-
'Waislamu ifanyeni Sweden ijute kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu'
Jul 21, 2023 07:39Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ameilaani serikali ya Sweden kwa kuruhusu kuvunjiwa heshima tena Qur'ani Tukufu na amewataka Waislamu duniani kuchukua hatua za kuifanya nchi hiyo ya Ulaya Magharibi ijute kwa jinai yake hiyo.
-
Iran yafanya maandamano ya nchi nzima kulaani kuvunjiwa heshima tena Qur'ani Tukufu nchini Sweden
Jul 21, 2023 07:39Wananchi Waislamu wa Iran leo wamefanya maandamano ya nchi nzima baada ya Sala za Ijumaa kulaani kuvunjiwa heshima tena Qur'ani Tukufu nchini Sweden kwa ulinzi kamili wa jeshi la polisi la nchi hiyo ya Ulaya Magharibi.
-
Iran: Mkuu wa UN achukue msimamo mkali dhidi ya kuvunjiwa heshima Qurani
Jul 21, 2023 04:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemuandikia barua Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akimtaka achukue msimamo mkali dhidi ya vitendo vya kuvunjiwa heshima Qurani Tukufu.
-
Iran yamuita balozi wa Sweden kulalamikia kuvunjiwa heshima Qurani
Jul 21, 2023 00:07Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imemuita balozi wa Sweden mjini Tehran kulalamikia hatua ya serikali ya nchi hiyo ya Ulaya Magharibi ya kuruhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.
-
Amir Abdollahian: Tumepokea mapendekezo ya Oman ili kurejesha pande zote katika JCPOA
Jul 20, 2023 08:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuhusu mazungumzo yake na mwenzake wa Oman kwamba: Muscat inafanya juhudi za kukurubisha mitazamo ili pande zote husika zirejee katika utekelezaji wa majukumu yake katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Iran yataka kutokomezwa mfumo wa apartheid Palestina
Jul 19, 2023 09:15Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kusambaratisha mfumo wa ubaguzi wa rangi (apartheid) kote duniani na hususan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Waziri wa Ulinzi: Hakuna anayeweza kuitishia Iran yenye nguvu
Jul 19, 2023 08:09Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu hivi sasa ina nguvu na uwezo mkubwa wa kiulinzi, na kwamba hakuna yeyote anayeweza kulitishia taifa hili.
-
Abdollahian: Kusifanywe jambo ambalo litatoa pigo kwa uhusiano wa Iran na Russia
Jul 19, 2023 04:31Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, kujitawala na mamlaka ya ardhi yote ya Iran ni jambo ambalo katu si kitu cha kufanyiwa mazungumzo.
-
Ubalozi wa Iran nchini Denmark: Kuvunjia heshima vitabu vitakatifu ni ukiukaji wa haki za binadamu
Jul 18, 2023 04:50Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Copenhagen, Denmark, umetaja vitendo vya kuchoma moto vitabu vitakatifu vya dini tofauti kuwa ni ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu.