Jul 19, 2023 08:01 UTC
  • Abdollahian: Kusifanywe jambo ambalo litatoa pigo kwa uhusiano wa Iran na Russia

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, kujitawala na mamlaka ya ardhi yote ya Iran ni jambo ambalo katu si kitu cha kufanyiwa mazungumzo.

Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Sergei Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia na kusisitiza ulazima wa kuheshimiwa mamlaka ya kujitawala na ardhi za mataifa mengine.

Hivi karibuni Moscow ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa mazungumzo ya kistratejia kati ya Russia na nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi uliohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman na Katibu Mkuu wa baraza la hilo. 

Baada ya mkutano huo, Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi na Russia zilitoa taarifa ya pamoja, na kwa mara nyingine tena katika sehemu moja ya taarifa hiyo kulikaririwa madai kuhusu visiwa hivyo vitatu vya Iran.  

Akijibu manung'uniko ya mwenzake wa Iran, Sergei Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema, Moscow haina shaka yoyote kuhusiana na mamlaka ya ardhi yote ya Iran na kwamba, inaheshimu kikamilifu misimamo ya Iran katika uwanja huo.  

Ikumbukwe kuwa, nyaraka zenye itibari ya kimataifa zinathibitisha kuwa, visiwa vitatu vya Bu Musa, Tombu Ndogo na Tombu Kubwa katika Ghuba ya Uajemi ni mali ya Iran. Kwa mfano, ramani ya jeshi la majini la Uingereza mnamo mwaka 1881 inaonyesha ramani ya Wizara ya Masuala ya Bahari ya Uingereza ya mwaka 1863.

Tags