-
Mabaharia 16 Wairani waachiliwa huru Tanzania
Nov 13, 2022 01:16Mabaharia 16 Wairani waliokuwa wanashikiliwa nchini Tanzania wameachiliwa huru hivi karibuni. Hayo yamedokezwa na Mkuu wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran katika Eneo la Biashara Huria la Chabahar katika mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini-mashariki mwa Iran ambaye amesema mabaharia hao walioachiliwa huru ni wenyeji wa mkoa wa Sistan na Baluchestan.
-
Bidhaa za Iran zinazidi kupata umaarufu barani Afrika
Nov 13, 2022 01:11Kaimu Mkuu wa Kituo cha Biashara ya Iran na Afrika amesema: "Inatabiriwa kuwa kwa kasi ya sasa ya ustawi wa biashara ya Iran na Afrika katika mwaka huu (1401 Hijria Shamsia) kiwango cha mauzo ya bidhaa za Iran barani Afrika kitafika dola bilioni 1.8.
-
Mashinikizo mapya ya Magharibi dhidi ya Iran baada ya kushindwa mradi wa kuibua ghasia
Nov 12, 2022 22:52Nchi za Magharibi baada ya kushindwa mradi wao wa kuibua ghasia nchini Iran sasa zinatafuta njia nyingine mpya mbadala ili kuiwekea mashinikizo Tehran. Katika uwanja huo, nchi za Magharibi khususan za Ulaya mbali na kuratibu vikwazo vipya zimejielekeza katika kutoa taarifa na maazimio dhidi ya Iran sambamba na kushadidisha mashinikizo ya kisiasa dhidi ya nchi hii.
-
Amir Abdollahian: Azimio la UN haliizuia Iran kuuza silaha nje ya nchi
Nov 12, 2022 04:40Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema: "Kwa mujibu wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama, hakuna marufuku ya kuagiza na kuuza silaha za Iran nje ya nchi, na Tehran haijaipa Russia silaha zozote ili zitumike katika vita vya Ukraine."
-
Jenerali Salami: Iran haitafumbia macho jinai za maadui
Nov 11, 2022 23:04Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu haitoacha jinai za maadui zipite hivi hivi bila ya kupewa majibu makali.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Uwezo wa makombora wa Iran ni wa utaalamu wa ndani na uzuiaji hujuma
Nov 11, 2022 08:36Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema, kuifanya sekta ya ulinzi ya makombora itegemee kikamilifu uwezo na utaalamu wa ndani kumeipa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nguvu za kumhofisha adui asiweze kuanzisha mashambulio.
-
Iran yasisitiza sera zake za kuwa na uhusiano na ujirani mwema na majirani zake.
Nov 11, 2022 03:19Nasser Kanaani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huku akijibu madai ya hivi karibuni ya Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan kuhusiana na eti uungaji mkono wa Iran kwa Armenia, amesisitiza kuwa sera kuu za Iran zimejengeka katika msingi wa kuwa na ujirani mwema na kupanua mahusiano na majirani wake wote na kuwa kuimarisha uhusiano na mmoja wa majirani hao hakuna maana ya kufanya uadui na majirani wengine.
-
Rais Raisi: Adui amefeli kuidhoofisha Iran kama alivyoshindwa katika kampeni ya vikwazo
Nov 10, 2022 23:40Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema njama ya adui ya kuzua ukosefu wa utulivu nchini Iran imefeli sawa na ilivyoshindwa sera ya vikwazo vikali dhidi ya nchi hii.
-
Onyo la Iran kwa Uingereza kwa vitendo vyake vya kiharibifu humu nchini
Nov 10, 2022 23:36Waziri wa Usalama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, katika matukio ya hivi karibuni ya humu nchini, "mkono wa utawala wa Kizayuni katika utekelezaji, mkono wa Uingereza katika propaganda na mkono wa utawala wa kiimla wa Aal Saud katika kugharamia machafuko, imeonekana wazi zaidi."
-
Iran yaunda kombora la balestiki la Hypersonic
Nov 10, 2022 07:57Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC ametangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kuzalisha kombora la balestiki la Hypersonic, lenye uwezo wa kupenya mifumo yote ya ngao ya ulinzi wa makombora duniani.