-
Iran yaionya Ujerumani: Jibu letu kwa uingiliaji wenu litakuwa zito
Nov 10, 2022 07:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali matamshi ya uingiliaji na ya kichochezi yaliyotolewa na mwenzake wa Ujerumani na kuonya kuwa, Tehran itatoa jibu lenye mlingano na madhubuti kwa misimamo hiyo ya uingiliaji wa masuala ya ndani ya nchi hii.
-
Abdollahian: Siasa za Iran za kukomeshwa vita vya Ukraine hazibadiliki
Nov 10, 2022 04:16Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, siasa za kimsingi na zisizobadilika za Jamhuri ya Kiislamu ni kuhitimishwa vita vya Ukraine.
-
Raisi: Ushirikiano wa nchi huru ndio jibu kwa mkakati wa Marekani wa kudhoofisha usalama
Nov 09, 2022 12:06Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, ushirikiano wa nchi huru ndilo jibu muhimu zaidi kwa stratijia ya Marekani ya kuyumbisha usalama.
-
Sisitizo jingine la Marekani la kuunga mkono vurugu na machafuko nchini Iran
Nov 09, 2022 05:12Ned Price, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani ameendelea kuunga mkono vurugu na machafuko nchini Iran na kukana kabisa kuhusika nchi yake katika vurugu hizo.
-
Iran: Majibu yetu kwa uvamizi wa maadui yatakuwa makali sana
Nov 09, 2022 03:48Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu la Iran ametoa onyo kali kwa maadui na kuwaambia: Mnapaswa kuelewa vyema kwamba iwapo mtafanya kosa lolote dhidi ya Iran ya Kiislamu, basi majibu mtakayopata yatakuwa makali sana.
-
Marandi: Matamshi ya Biden dhidi ya Iran ni juhudi za mfa maji
Nov 08, 2022 23:38Mshauri wa timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran amejibu matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Rais wa Marekani akiigilia kati masuala ya ndani na matukio ya hivi karibuni nchini Iran, na ameyataja matamshi hayo kuwa ni "juhudi za mfa maji".
-
Kulaaniwa hujuma za kigaidi nchini Iran; ulazima wa kukabiliana na Daesh na tawala za kihalifu
Nov 08, 2022 08:54Jumuiya ya Kimataifa ya Kutetea Wahanga wa Ugaidi imetoa taarifa inayolaani hujuma za kigaidi za hivi karibuni dhidi ya vikosi vya usalama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran: Tutapambana vilivyo na magaidi wote wanaohatarisha usalama wetu
Nov 08, 2022 07:51Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), amewatembelea hospitalini maafisa wa polisi waliojeruhiwa katika machafuko ya hivi karibuni humu nchini na kusisisitiza kuwa Tehran itapambana vilivyo na magaidi wanaohatarisha usalama wa nchi.
-
Iran yaipa mkono wa pole Tanzania kwa vifo vya watu waliofariki katika ajali ya ndege
Nov 07, 2022 23:36Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na wananchi wa Tanzania kufuatia ajali ya ndege iliyosababisha vifo vya raia kadhaa wa nchi hiyo.
-
Iran yawakamata magaidi 26 waliohusika na hujuma Shiraz
Nov 07, 2022 23:02Wizara ya Intelijensia ya Iran imesema kuwa, vikosi vya usalama nchini vimewatia mbaroni magaidi 26 wakufurishaji ambao waliuhusika na shambulio la hivi karibuni la kigaidi kwenye Haram Takatifu ya Shah Cheragh katika mkoa wa kusini wa Fars na kuongeza kuwa, mratibu mkuu wa machafuko hayo hatari ni raia wa Jamhuri ya Azerbaijan.