Abdollahian: Siasa za Iran za kukomeshwa vita vya Ukraine hazibadiliki
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, siasa za kimsingi na zisizobadilika za Jamhuri ya Kiislamu ni kuhitimishwa vita vya Ukraine.
Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiiislamu ya Iran amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na mwenzake wa Italia Antonio Tajani na kubainisha kwamba, ni kwa msingi huo ndio maana Tehran inaendelea na juhudi zake za kusaidia mchakato wa kisiasa.
Katika mazungumzo yake hayo na Antonio Tajani, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Italia, Amir Abdollahian amebadilishana mawazo pia na mwenzake huyo kkuhusiana na ushirikiiano wa pande biili na namna ya kupanua ushirikkiano zaidi katiika nyuga mbalimbali.
Hivi karibuni pia Amir-Abdollahian aligusia matukio ya karibuni nchini Ukraine na madai yaliyotolewa na baadhi ya maafisa wa nchi hiyo kwamba ndege zisizo na rubani za Iran ambazo ilipatiwa Russia tokea miaka kadhaa nyuma zimetumika katika vita dhidi ya Ukraine na akasema: "sisi tunapinga vikali vita na kuupatia silaha upande wowote kati ya pande mbili zinazopigana, na tumewaeleza viongozi wa Ukraine kwamba kama wana ushahidi wowote kuhusiana na kutumiwa ndege zisizo na rubani za Iran katika vita dhidi ya nchi hiyo, waonyeshe".
Tarehe 24 Februari mwaka huu wa 2022, Russia ilianzisha kampeni maalumu ya kijeshi baada ya kuchochewa na Jeshi la Nchi za Magharibi NATO ambalo liliendelea kurundika wanajeshi wake kwenye mipaka ya Russia na kudharau maonyo yote ya mara kwa mara yaliyotolewa na viongozi wa Moscow.