Pars Today
Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekanusha tuhuma dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu zilizotolewa na Marekani na Uingereza za eti kuvuruga amani katika eneo la Asia Magharibi na kuhusika na mapigano yanayoendelea Ukraine; akisisitiza kuwa tuhuma zote hizo hazina msingi wowote.
Rais Vladimir Putin wa Russia Jumanne, Novemba 19, alitia saini amri ambayo inaipa Moscow ruhusa ya kutumia silaha za nyuklia dhidi ya "nchi isiyo na silaha za nyuklia" ilimradi nchi hiyo iwe inaungwa mkono na nguvu za nyuklia.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuzuia kuongezeka mapigano nchini Ukraine.
Rais Xi Jinping wa China ameweka wazi mistari myekundu minne ambayo amesema haipasi kuvukwa na Marekani ili kuwepo uhusiano wenye usawa na sahihi kati ya nchi hizo mbili.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ametahadharisha kuhusu Ufaransa kutuma makombora nchini Ukraine.
Kansela wa Ujerumani amesema kuwa anahitilafiana pakubwa kimitazamo na Waziri Mkuu wa Hungary kuhusu namna ya kushughulikia mgogoro wa Ukraine na kukiri kuwepo hitilafu hizo ndani ya Umoja wa Ulaya kuhusu Ukraine.
Rais wa Uturuki amesema kuwa, ingawaje Marekani ndiye mpinzani mkuu wa Ukraine kujiunga na Shirika la la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO), lakini pia nchi nyingi za jumuiya hiyo zinapinga Kyev kupewa uanachama.
Rais Vladimir Putin wa Russia ameamuru mwongozo wa utumiaji silaha za nyuklia wa nchi hiyo ufanyiwe mabadiliko akionya pia kuwa nchi yake inaweza kujibu mapigo kwa silaha za nyuklia ikiwa itashambuliwa kwa silaha za kawaida zilizotolewa na dola linalomiliki silaha hizo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa Umoja wa Ulaya unapasa kujiepusha na kutoa tuhuma kwa kutegemea taarifa za uongo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu haina mchango wowote katika vita vinavyoendelea kati ya Russia na Ukraine, na daima imekuwa ikikariri wito wake wa mazungumzo ya kuutafutia ufumbuzi mzozo huo.