-
Iran yaonya kuhusu kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu duniani
Jun 20, 2022 22:52Balozi wa mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ametoa indhari kuhusu kuongezeka vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia.
-
Iran yakamata tani moja na nusu ya mihadarati kusini mashariki mwa nchi
Jun 20, 2022 07:39Kamanda wa jeshi la Polisi la Mkoa wa Sistan na Baluchistan wa kusini mashariki mwa Iran ametangaza kuwa, jeshi hilo limekamata karibu tani moja na nusu ya madawa ya kulevya kwenye eneo hilo.
-
Hatua mpya za kustawisha uhusiano wa Iran na Kazakhstan
Jun 20, 2022 04:50Hati tisa za maelewano na waraka wa ushirikiano kati ya Iran na Kazakhstan zimesainiwa hapa Tehran katika hafla iliyohudhuriwa na marais wa nchi hizo mbili.
-
Iran inabeba mzigo mkubwa zaidi wa wakimbizi katika eneo
Jun 20, 2022 03:08Mwakilishi maalumu wa Jamhuri ya Kiislamu y Iran katika masuala ya Afghanistan amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kutokana na vigezo vyake vya Kiislamu na kibinaadamu imekubali kubeba mzigo mkubwa zaidi wa wakimbizi katika eneo.
-
Kiongozi Muadhamu: Tatizo kuu katika kadhia ya Ukraine ni mpango wa nchi za Magharibi kupanua NATO
Jun 19, 2022 23:07Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutana na Rais wa Kazakhstan na kusema tatizo kuu katika kadhia ya Ukrain ni kuwa, nchi za Magharibi zina mpango wa kupanua muungano wa kijeshi wa NATO.
-
Iran na Kazakhstan kuimarisha uhusiano, zasaini hati 9 za maelewano na ushirikiano
Jun 19, 2022 08:23Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran na Kazakhstan zimekuwa na uhusianio mzuri kwa miaka 30 iliyopita lakini uhusiano huu hautoshi.
-
Iran: Utawala wa Kizayuni ndiyo sababu ya ugaidi na uharibifu katika eneo hili zima
Jun 19, 2022 02:26Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema katika mazungumzo yake na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) kwamba kuwepo utawala pandikizi wa Kizayuni katika eneo hili ndiyo sababu ya ukosefu wa utulivu na amani kama ambavyo ndio ulioleta vitendo vya kigaidi na uharibifu katika eneo hili zima.
-
Waziri wa Ulinzi asisitiza kuongezwa uwezo wa jeshi la majini la Iran kulingana na ukubwa wa vitisho
Jun 19, 2022 01:15Akiwa ziarani katika mkoa wa Hormozgan kusini mwa Iran, Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametembelea miradi ya majini ya wizara hiyo huko Bandar Abbas hususan utengenezaji wa manowari, meli za kawaida za kivita na nyambizi na kusema kuwa kuimarishwa nguvu katika pande zote za ulinzi ikiwa ni pamoja na nchi kavu anga, na hasa baharini, ni moja ya vipaumbele vya mipango ya ulinzi wa nchi.
-
Watalii wa kigeni waongezeka Iran, waingiza pato la dola bilioni 2.3
Jun 18, 2022 22:17Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema sekta ya utalii inazidi kuimarika humu nchini ambapo katika kipindi cha mwaka moja uliopita watalii wa kigeni wametumia dola bilioni 2.5 wakiwa ndani ya Iran.
-
Iran: Tumeitaarifu IAEA kuhusu shughuli zetu katika kituo cha nyuklia cha Natanz
Jun 18, 2022 08:02Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema Jamhuri ya Kiislamu imelitaarifu Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) kuhusu mpango wake wa kuhamishia mji wa Natanz katikati ya Iran, shughuli za kituo cha nyuklia cha TESA kilichoko katika mji wa Karaj, viungani mwa mji mkuu Tehran.