-
Iran na EU zajadili namna ya kuondolewa vikwazo vyote haramu katika JCPOA
Oct 27, 2021 10:28Ofisi ya uwakilishi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Ulaya imetangaza kuwa, kuondolewa vikwazo vyote haramu na visivyo vya kisheria ilivyoekewa Iran ndio ajenda kuu ya mazungumzo ya Brussels kati ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa na mratibu wa kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Mkutano wa pili wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa mataifa jirani na Afghanistan+Russia waanza Tehran
Oct 27, 2021 04:42Mkutano wa pili wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa mataifa jirani na Afghanistan+Russia umeanza kufanyika hapa mjini Tehran kwa shabaha ya kujadili changamoto mbambali zinazoikabili nchi hiyo baada ya majeshi ya Marekani kuondoka nchini humo na wanamgambo wa Taliban kuchukua hatamu za uongozi wa nchi.
-
Rais wa Iran afanya mazungumzo na Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Tajikistan, Turkemanistan, Uzibekistan na Pakistan
Oct 27, 2021 00:41Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo hapa mjini Tehran na Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Pakistan, Uzbekistan, Tajikistan na Turkemanistan walioko hapa nchini kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi jirani na Afghanistan kinachofanyika leo Jumatano hapa Tehran.
-
Iran: Tunaendelea kufanya mashauriano ya kiusalama na serikali mpya ya Afghanistan
Oct 26, 2021 08:57Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inaendelea kufanya mashauriano na serikali mpya ya Afghanistan hasa katika masuala ya kuleta amani, utulivu na usalama wa kudunu nchini humo.
-
Rais wa Iran azitaka nchi za za Ulaya zisikubali mashinikizo ya Marekani
Oct 26, 2021 01:02Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito kwa nchi za Ulaya kukataa mashinikizo ya Marekani wakati zinapojichukulia maamuzi.
-
Rais wa Iran ayataka madola ya Ulaya kuwa na mamlaka katika kuchukua maamuzi
Oct 25, 2021 07:26Rais Ibrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kusisitiza kuwa, madola ya Ulaya yanapaswa kuwa na mamlaka katika kuchukua maamuzi amesema kuwa, maataifa hayo hayapaswi kufanya mambo kwa namna ambayo yataifanya Marekani kuyaona kama sehemu yake ya kupenya na kupitishia mambo yake.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu kuhusu udharura wa kubainishwa umuhimu wa umoja katika Ulimwengu wa Kiislamu
Oct 25, 2021 07:00Akizungumza Jumapili kwa mnasaba wa kuzaliwa Mtume (saw) na mjukuu wake Imam Jaffar as-Swadiq (as) mbele ya hadhara ya viongozi wa ngazi za juu wa mfumo wa Kiislamu na wageni walioshiriki katika kikao cha kimataifa cha Wiki ya Umoja wa Kiislamu hapa mjini Tehran, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema umoja wa Kiislamu ni msingi na faradhi ya Kiislamu na kwamba lengo kuu la utamaduni mpya wa Kiislamu haliwezi kufikiwa bila kuwepo umoja wa Shia na Suni.
-
Shamkhani: Israel itenge bajeti ya kutosha ya kukarabati hasara za majibu ya Iran
Oct 24, 2021 23:04Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel uanze kufikiria kutenga bajeti ya hasara kubwa zitakazosababishwa na majibu makali ya Iran.
-
Kiongozi Muadhamu: Mazazi ya Mtume (SAW) yalifungua ukurasa mpya wa maisha ya mwanadamu
Oct 24, 2021 11:47Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuzaliwa Mtume mtukufu Muhammad (SAW) kulifungua ukurasa mpya katika maisha ya mwanadamu.
-
Iran iko tayari kushirikiana na nchi za Kiislamu katika uga wa nyuklia
Oct 24, 2021 11:43Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran (AEOI) amesema Jamhuri ya Kiislamu ipo tayari kushirikiana na nchi za Kiislamu katika sekta ya nishati ya nyuklia.