Rais wa Iran azitaka nchi za za Ulaya zisikubali mashinikizo ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i76174-rais_wa_iran_azitaka_nchi_za_za_ulaya_zisikubali_mashinikizo_ya_marekani
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito kwa nchi za Ulaya kukataa mashinikizo ya Marekani wakati zinapojichukulia maamuzi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 26, 2021 01:02 UTC
  • Rais wa Iran azitaka nchi za za Ulaya zisikubali mashinikizo ya Marekani

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito kwa nchi za Ulaya kukataa mashinikizo ya Marekani wakati zinapojichukulia maamuzi.

Rais Rais ameyasema hayo Jumatatu mjini Tehran wakati alipopokea vitambulisho vya mabalozi wapya wa Uswisi na Finland nchini Iran.

 Katika mkutano wake na balozi mpya wa Uswisi mjini Tehran, Raisi amesema uhusiano baina ya nchi hizi mbili daima umekuwa wa kirafiki na kuongeza kuwa: "Uswisi  daima imekuwa na nafasi chanya katika kustawisha amani na inatazamiwa kuwa itadumisha msimamo wake huru katika zama hizi mpya za sera za Marekani kujichukulia maamuzu ya upande mmoja."

Balozi mpya wa Uswisi naye  amesema Iran ni nchi kongwe yenye ustaarabu ulionawiri na kuongeza kuwa kwa muda wa miaka 100,  Iran na Uswisi zimekuwa na uhusiano mzuri wa kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi na kisayansi. 

Rais Ebrahim Raisi wa Iran

 

Ikumbukwe kuwa baada ya uhusiano wa kidiplomasia bainaya Iran na Marekani kusitishwa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979, ubalozi wa Uswisi mjini Tehran husimamia masuala ya kidiplomasia yanayohusiana na Marekani na pia huwapa huduma raia wa Marekani wanaosafiri au kuishi Iran.

Wakati huo huo, Rais Raisi amepokea pia vitambulisho vya balozi mpya wa Finland mjini Tehran na kusisitiza kuwa nchi za Ulaya zinapaswa kujiweka kando na sera za kujitanua za Marekani kwani sera hizo si kwa maslahi ya dunia.

Aidha amesema uhusiano wa Iran na Finland ni mzuri na amebainisha matumaini yake kuwa uhusiano huo utaboreka wakati wa balozi mpya.