-
Iran na Uturuki; ulazima wa kufanyika juhudi za kuboresha uhusiano wa kiuchumi
Oct 24, 2021 06:57Katika siku za hivi karibuni maafisa na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamuu ya Iran na Uturuki wamekuwa na mazungumzo ya pande mbili ya ana kwa ana na kwa njia ya simu ambapo wamekuwa wakisisitizia udharura wa umuhimu wa uhusiano wa nchi mbili katika nyanja za kiuchumi na ushirikiano wa kieneo kwa shabaha ya kuleta amani na uthabiti, na wakati huo huo kuzuia hatua zozote zile zenye lengo la kuleta mizozo na mivutano.
-
Spika wa Bunge la Iran awapongeza maspika wa nchi za Kiislamu kwa mnasaba wa Maulidi ya Mtume (saw)
Oct 24, 2021 04:45Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amewatumia ujumbe maspika wenzake katika nchi za Kiislamu akiwapa mkono wa kheri na baraka kwa mnasaba wa maadhimisho na sherehe za Maulidi ya Mtume Muhammad (saw).
-
Amir-Abdollahian: Mazungumzo ya nyuklia na kundi la 4+1 yataanza tena hivi karibuni
Oct 24, 2021 01:03Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mazungumzo ya nyuklia na kundi la 4+1 yanatarajiwa kuanza tena hivi karibuni.
-
Rais wa Iran atuma salaamu maalumu za Maulidi na kuzaliwa Mtume (saw) kwa viongozi wa nchi za Kiislamu
Oct 23, 2021 23:55Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Ebrahim Raisi ametuma salamu maalumu na mkono wa baraka na fanaka kwa viongozi wa nchi za Kiislamu kwa mnasaba wa maadhimisho ya Maulidi na siku ya kuzaliwa Mtume wa Mwisho wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (saw) na Wiki ya Umoja wa Kiislamu.
-
Mwanazuoni wa Kisunni Iran asisitiza kuhusu umoja wa Waislamu
Oct 23, 2021 08:19Mkrugenzi wa Chuo cha Kidini cha Ahul Sunna cha Al Ahnafekhaf katika mkoa wa Khorassan Razavi kaskazini mashariki mwa Iran amesisitiza kuhusu ulazima wa kulinda umoja na mshikamano baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni ili kuvunja njama za maadui.
-
Swala ya Ijumaa Tehran yafanyika baada ya kusimamishwa kwa miezi 20 kutokana na corona
Oct 22, 2021 11:19Baada ya kusimamishwa kwa kipindi cha miezi ishirini jijini Tehran na katika miji na maeneo mengine ya Iran kutokana na maambukizi ya virusi vya corona, Swala ya Ijumaa imefanyika leo mjini Tehran ikishirikisha matabaka mbalimbali ya wananchi.
-
Gallop: Asilimia 72 ya watu wa Iran wanaridhishwa na utendaji wa serikali ya Raisi
Oct 22, 2021 06:45Kwa mujibu wa takwimu za karibuni za matokeo ya uchunguzi wa maoni, asilimia 72 ya wananchi wa Iran wanaridhishwa na utendahi wa serikali ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wanaiunga mkono kikamilifu.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Uturuki waelezea wasiwasi kuhusu kuongezeka ugaidi wa Daesh Afghanistan
Oct 22, 2021 06:24Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki wamebainisha wasiwasi wao kuhusu kuongezeka vitendo vya ugaidi wa Daesh dhidi ya waumini katika misikiti ya Afghanistan ambavyo hadi sasa vimepelekea kuuawa makumi ya waumini waliokuwa wakitekeleza ibada ya swala ya Ijumaa katika misikiti hiyo.
-
Washindi wa Tuzo ya Mustafa SAW 2021 watunukiwa zawadi mjini Tehran
Oct 22, 2021 00:25Wanasayansi watano Waislamu wametunukiwa zawadi ya Tuzo ya Mustafa SAW ya mwanasayansi bora katika Ulimwengu wa Kiislamu mwaka huu wa 2021.
-
Iran yatoa huduma za kitiba kwa waliojeruhiwa katika mlipuko msikitini Afghanistan
Oct 21, 2021 08:03Raia wa Afghanistan ambao walijeruhiwa katika hujuma ya kigaidi dhidi ya msikiti Ijumaa katika mji wa Kandahar wamefikishwa mjini Tehran kwa ajili ya matibabu.