Mwanazuoni wa Kisunni Iran asisitiza kuhusu umoja wa Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i76082-mwanazuoni_wa_kisunni_iran_asisitiza_kuhusu_umoja_wa_waislamu
Mkrugenzi wa Chuo cha Kidini cha Ahul Sunna cha Al Ahnafekhaf katika mkoa wa Khorassan Razavi kaskazini mashariki mwa Iran amesisitiza kuhusu ulazima wa kulinda umoja na mshikamano baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni ili kuvunja njama za maadui.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 23, 2021 08:19 UTC
  • Mwanazuoni wa Kisunni Iran asisitiza kuhusu umoja wa Waislamu

Mkrugenzi wa Chuo cha Kidini cha Ahul Sunna cha Al Ahnafekhaf katika mkoa wa Khorassan Razavi kaskazini mashariki mwa Iran amesisitiza kuhusu ulazima wa kulinda umoja na mshikamano baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni ili kuvunja njama za maadui.

Kwa mujibu wa taarifa, Mawlana Habiburahman Mutahhari Mkurugenzi wa Chuo cha Kidini  cha Al Ahnafekhaf  amesema, maadui na mabeberu wa kimataifa wanaibua mifarakano na ugomvi baina ya Waislamu ili kufikia malengo yao haramu na hivyo umoja na mashikamano wa Shia na Sunni ni dharura katika kusambaratisha njama hii ya maadui.

Mawlana Mutahhari amesema iwapo Waislamu watadumisha mshikamano baina yao na kuishi kwa maelewano, basi maadui hawataweza kutoa pigo kwa Waislamu na Uislamu.

Mkrugenzi wa Chuo cha Kidini cha Ahul Sunna cha Al Ahnafekhaf aidha amesema umoja na mshikamano wa Waislamu wote si kwa ajili ya eneo au nchi maalumu.

Moulana Mutahhari aidha amesema umoja ni dharura ya kidini, kijamii na kisiasa katika jamii za Kiislamu na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla na kuongeza kuwa: "Waislamu wawe ni wa madhehebu ya Shia au Sunni wanapaswa kushirikiana na kuelewana na kutafuta nukta za pamoja baina yao huku wakijepusha na kila aina ya mifarakano ambayo ni kwa maslahi ya maadui."