-
Iran yatoa huduma za kitiba kwa waliojeruhiwa katika mlipuko msikitini Afghanistan
Oct 21, 2021 08:03Raia wa Afghanistan ambao walijeruhiwa katika hujuma ya kigaidi dhidi ya msikiti Ijumaa katika mji wa Kandahar wamefikishwa mjini Tehran kwa ajili ya matibabu.
-
Iran yaanza mazoezi makubwa ya kijeshi angani
Oct 21, 2021 07:58Kikosi cha Anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimeanza mazoezi makubwa yaliyopewa jina la 'Duru ya 10 Uwezo wa Anga wa Waliojitolea Kulinda Anga ya Wilayat'. Mazoezi hayo yamezinduliwa rasmi kwa kutamkwa ' Ya Muhammad Rasulullah SAW.
-
Raisi Ebrahim Raisi: Stratijia ya Iran ni kuwepo umoja baina ya Waislamu
Oct 21, 2021 04:28Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, stratijia ya Iran ni kuhakikisha kwamba kunakuwepo umoja na mshikamano katika Ulimwengu wa Kiislamu.
-
Ayatullah Jannati: Tunakaribisha kwa mikono miwili mazungumzo ya Iran na Saudi Arabia
Oct 20, 2021 22:52Ayatullah Ahmad Jannati, Katibu wa Baraza la Kulinda Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu ni ya kutwishwa na ni matakwa ya mabeberu dhidi ya Uislamu.
-
Mkutano wa 35 wa Umoja wa Kiislamu, mwelekeo na malengo
Oct 20, 2021 22:51Mkutano wa 35 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu ulianza Jumanne ya wiki hii mjini Tehran kwa hotuba ya Rais Sayyid Ebrahim Raisi ukijadili maudhui ya umoja wa Kiislamu, amani na kujiepusha na mifarakano na mizozo katika Ulimwengu wa Kiislamu. Mkutano huo ni sehemu ya sherehe za Maulidi na kumbukumbu ya kuzaliwa mbora wa viumbe na Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (saw).
-
Mufti Mkuu wa Croatia: Mkutano wa Umoja wa Kiislamu ni kiriri cha kuelezea hali ya nchi za Kiislamu
Oct 20, 2021 09:57Mufti Mkuu wa Waislamu wa Croatia amesema, Mkutano wa Umoja wa Kiislamu ni kiriri cha kuelezea hali ya sasa ya nchi za Kiislamu.
-
Kasi ya chanjo nchini Iran yawashangaza Wamagharibi
Oct 20, 2021 03:51Kasi kubwa ya zoezi la kudunga chanjo ya COVID-19 nchini Iran imezishangaza sana nchini za Magharibi.
-
Washiriki wa Mkutano wa Wiki ya Umoja wahimiza kulindwa vilivyo mshikamano wa Waislamu
Oct 19, 2021 23:19Watoa hotuba katika kikao cha ufunguzi cha 35 cha Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu wametilia mkazo sana wajibu wa kushikamana na kuwa kitu kimoja Waislamu na kukabiliana vilivyo na njama za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel za kujaribu kuzusha mifarakano kati ya nchi za Waislamu.
-
Sisitizo la Iran la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuwa na mchango amilifu zaidi nchini Afghanistan
Oct 19, 2021 22:51Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, lengo la genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh huko Afghanistan ni kuchochea chuki na uadui wa kimadhehebu na ameitaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ilaani vikali vitendo vya kinyama vya Daesh.
-
"Kuzikurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu ni hatua ya kistratajia"
Oct 19, 2021 10:09Rais wa Iran amesema wazo la kuzikurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu lililobuniwa na Imam Khomeini (MA), Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ni hatua ya kistratajia katika ulimwengu wa Kiislamu.