-
Iran: Mabadilishano ya wafungwa yasihusishwe na mazungumzo ya JCPOA
Oct 19, 2021 09:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran inalitazama suala la kubadilishana wafungwa kuwa la kibinadamu, na haitaki kuona likifungamanishwa na mazungumzo ya nyuklia ya JCPOA.
-
Mkutano wa Kimataifa wa Umoja baina ya Waislamu waanza mjini Tehran
Oct 19, 2021 04:39Kwa mnasaba wa kuanza Wiki ya Umoja, mkutano wa 35 wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza leo hapa mjini Tehran kwa kaulimbiu ya "Umoja wa Kiislamu; Amani na Kuepukana na Mifarakano."
-
Rais Raisi: Tuna nia ya dhati ya kufanya mazungumzo ya nyuklia lakini yenye tija
Oct 18, 2021 23:46Rais Ebrahim Raisi amesema, Iran haijawahi katu kujiondoa kwenye meza ya mazungumzo na ina nia ya dhati ya kufanya mazungumzo lakini yenye tija na akabainisha kuwa, mazungumzo ya nyuklia inapasa yawe na natija; na upande wa pili uonyeshe utayarifu wa dhati wa kufuta vikwazo.
-
Iran yaitaka OIC ilaani mashambulio ya kigaidi ya ISIS nchini Afghanistan
Oct 18, 2021 21:15Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa lengo la genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) huko Afghanistan ni kuchochea chuki na uadui wa kimadhehebu na ameitaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ilaani vikali vitendo vya kinyama vya Daesh.
-
Mohseni-Eje'i : Iran itawafuatilia na kuwatia adabu waliohusika na mauaji ya kigaidi ya Kamanda Soleimani
Oct 18, 2021 07:56Mkuu wa Idara wa Mahakama nchini Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itawafuatilia na kuwaadhibu wale wote waliohusika na mauaji ya kigaidi ya Kamanda Luteni Jenerali Qassem Soleimani.
-
Wanafunzi, wanavyuoni wa kidini Iran walaani mauaji ya Waislamu Afghanistan
Oct 18, 2021 00:22Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Kidini katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran wamefanya maandamano makubwa ya kulaani ongezeko la mashambulio ya kigaidi yanayolenga misikiti ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Afghanistan.
-
Qalibaf: Marekani inaendeleza hatua za kuibua mivutano magharibi mwa Asia
Oct 17, 2021 04:18Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesisitiza kuwa, hatua za Marekani za kuibua mivutano magharibi mwa Asia zingali zinaendelea.
-
Iran yajibu madai ya rais wa Jamhuri ya Azerbaijan
Oct 16, 2021 03:52Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Iran ameyataja kuwa ya kustaajabisha na bandia madai mapya ya rais wa Jamhuri ya Azerbaijan dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao cha viongozi wa Jumuiya ya Madola ya Nchi Huru (CIS) na kusema Iran inakanusha vikali mada hayo.
-
Iran yasisitiza umoja wa Shia-Sunni katika kukabiliana na njama za maadui wa Waislamu
Oct 16, 2021 01:08Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali kitendo cha magaidi wakufurishaji kuushambulia msikiti wa Bibi Fatima wakati wa Sala ya Ijumaa mjini Kandahar nchini Afghanistan.
-
Salami: Kikosi cha Majini cha IRGC kina uwezo wa kujibu haraka chokochoko
Oct 15, 2021 23:01Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kikosi cha baharini cha jeshi la SEPAH kimefikia upeo wa juu wa uwezo wa kujibu haraka tishio lolote la maadui.