Mkutano wa Kimataifa wa Umoja baina ya Waislamu waanza mjini Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i75924-mkutano_wa_kimataifa_wa_umoja_baina_ya_waislamu_waanza_mjini_tehran
Kwa mnasaba wa kuanza Wiki ya Umoja, mkutano wa 35 wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza leo hapa mjini Tehran kwa kaulimbiu ya "Umoja wa Kiislamu; Amani na Kuepukana na Mifarakano."
(last modified 2026-08-08T07:03:00+00:00 )
Oct 19, 2021 04:39 UTC
  • Mkutano wa Kimataifa wa Umoja baina ya Waislamu waanza mjini Tehran

Kwa mnasaba wa kuanza Wiki ya Umoja, mkutano wa 35 wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza leo hapa mjini Tehran kwa kaulimbiu ya "Umoja wa Kiislamu; Amani na Kuepukana na Mifarakano."

Mkutano huo wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu unaofanyika kwa kaulimbiu ya "Umoja wa Kiislamu; Amani na Kuepukana na Mifarakano na Mizozo katika Ulimwengu wa Kiislamu" umefunguliwa leo mjini Tehran kwa hotuba ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mkutano huo wa siku tano, ambao kwa sababu ya kuchunga miiko na miongozo ya kiafya ya kujiepusha na janga la corona unafanyika kwa mahudhurio ya moja kwa moja na kwa njia ya intaneti, unahudhuriwa na washiriki kutoka Iran na nchi 39 duniani.

Rais Ebrahim  Raisi

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo, mbali na Rais Ebrahim Raisi, shakhsia wengine kadhaa wanatazamiwa kuhutubia pia, akiwemo Ziyad Nakhalah, Katibu Mkuu wa Jihadul-Islami ya Palestina, waziri mkuu wa zamani wa Iraq Adil al-Mahdi, Mufti wa Croatia Aziz Hasanvich, Mkuu wa masuala ya kimataifa wa Harakati ya Hamas Khalil al Hillah, Spika wa bunge la Algeria Bou Abdullah Bou Ghulamullah na wanafikra wengine kadhaa wa Ulimwengu wa Kiislamu.

Katika hafla hiyo ya leo kitazinduliwa pia kitabu cha Mawsuua'h cha majimui ya athari za Allamah Muhammad Taskhiri.../