Qalibaf: Marekani inaendeleza hatua za kuibua mivutano magharibi mwa Asia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i75844-qalibaf_marekani_inaendeleza_hatua_za_kuibua_mivutano_magharibi_mwa_asia
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesisitiza kuwa, hatua za Marekani za kuibua mivutano magharibi mwa Asia zingali zinaendelea.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 17, 2021 04:18 UTC
  • Qalibaf: Marekani inaendeleza hatua za kuibua mivutano magharibi mwa Asia

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesisitiza kuwa, hatua za Marekani za kuibua mivutano magharibi mwa Asia zingali zinaendelea.

Muhammad Baqir Qalibaf amesema leo katika kikao cha wazi cha bunge kuwa eneo la magharibi mwa Asia hii leo lipo katika hali nyeti sana na kwamba njama na mipango tete inatekelezwa ili kuzitumbukiza nchi za eneo hili katika vita vya ndani. 

Qalibaf ameongeza kuwa: Marekani na vibaraka wake wameliweka katika ajenda yao ya kazi suala la kuzusha hitilafu kati ya nchi za eneo ili kuzizuia nchi hizo kushirikiana kiuchumi na kuwa na amani ya kudumu katika eneo zima. 

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito kwa Wizara ya Mambo ya Nje kuchukua hatua za lazima na kutekeleza misimamo ya busara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mazingira nyeti ya sasa ili kudumisha amani na utulivu katika eneo.