-
Sayyid Ibrahim Raeisi aapishwa na kuwa Rais wa nane wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Aug 05, 2021 10:04Sayyid Ibrahim Raeisi amekula kiapo jioni ya leo na kuwa rais wa 8 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuahidi kwamba atalinda na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na Katiba ya nchi kwa nguvu zake zote.
-
Raeisi ataka kuimarishwa uhusiano wa Iran na nchi za Afrika
Aug 05, 2021 08:05Rais wa Iran amesema kiwango cha uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu na nchi za Afrika ikiwemo Ghana hakiridhishi na kwamba kuna haja ya kuimarishwa zaidi mahusiano hayo.
-
Raeisi: Uhusiano wa Tehran na Muscat umetokana na maingiliano na masuala ya kihistoria ya mataifa mawili
Aug 05, 2021 03:27Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa uhusiano wa Tehran na Muscat ni zaidi ya uhusiano wa nchi mbili jirani na umetokana na maingiliano na masuala ya historia baina ya nchi mbili.
-
Meja Jenerali Salami: Majibu yetu yatakuwa haribifu, ya kusambaratisha na ya kumfanya adui ajute
Aug 04, 2021 07:44Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) amezungumzia propaganda za vyombo vya habari vya maadui na kusema kuwa, maadui wanapaswa kutambua kwamba, majibu yetu yatakuwa haribifu, ya kusambaratisha na ya kuwafanya wajute.
-
Viongozi waalikwa waendelea kuwasili nchini kuhudhuria hafla ya kuapishwa rais mpya wa Iran
Aug 04, 2021 03:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Bosnia Herzegovina na waziri wa utalii wa Ghana wamewasili mjini Tehran kuhudhuria hafla ya kuapishwa rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran yakanusha uvumi kwamba vikosi vyake vya ulinzi vimeingia ndani ya meli zinazopita katika Ghuba ya Uajemi
Aug 03, 2021 22:32Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekanusha vikali madai ya baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi na vya Kizayuni vilivyodai kwamba vikosi vya ulinzi vya Iran vimeingia ndani ya meli zinazopita katika Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman.
-
CNN: Raeisi hatalegeza kamba hata kiduchu mbele ya Marekani
Aug 03, 2021 20:27Televisheni ya CNN ya Marekani imeripoti kwamba, kwa rais huyu mpya wa Iran, Tehran haitarudi nyuma hata kidogo mbele ya Marekani, na kuchaguliwa kwa Ebrahim Raeisi kuwa Rais wa Iran kutakuwa na matunda makubwa kwa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Raeisi: Tunataka kuondolewa vikwazo lakini hatutegemea madola ya kigeni
Aug 03, 2021 10:04Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa serikali yake inataka kuondolewa vikwazo haramu vilivyowekwa na madola ya kibeberu dhidi ya Iran lakini suala hilo halitafungamanishwa na matakwa ya madola ajinabi.
-
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu katika sherehe ya kuidhinishwa rasmi rais wa serikali ya 13; sisitizo la kulindwa thamani za Mapinduzi
Aug 03, 2021 06:58Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemuidhinisha rasmi Sayyid Ibrahim Raisi kuwa rais wa serikali ya 13 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sherehe maalumu iliyofanyika leo Jumanne katika Husainiya ya Imam Khomeini (MA) hapa mjini Tehran.
-
Kiongozi Muadhamu asisitiza udharura wa kutekelezwa vipaumbele vya serikali ya 13
Aug 03, 2021 03:20Sherehe za kuidhinishwa rasmi rais wa serikali ya 13 na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu zimefanyika leo mchana katika Hussainiya ya Imam Khomeini (MA) mjini Tehran ambapo Ayatullah Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Mfumo wa Kiislamu wamehudhuria kwa kuzingatia kikamilifu maelekezo na miongozo ya Wazara ya Afya juu ya kujikinga na virusi vya Covid-19.