-
Nguvu ya majini ya Iran; mseto wa nguvu za kijeshi, diplomasia, teknolojia na maadili ya kibinadamu
Feb 12, 2026 22:30Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, uwepo wa meli za Iran katika bahari na maji ya kimataifa ni mseto wa nguvu za kijeshi na diplomasia ya baharini.
-
Pezeshkian apongeza hamasa kubwa ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya tarehe 22 Bahman
Feb 12, 2026 07:54Rais Masoud Pezeshkian amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Iran kwa kujitokeza kwa wingi "katika hamasa ya aina yake" katika maandamano ya kitaifa kote nchini ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Araqchi: Wairani waliandamana tarehe 22 Bahman kutangaza kuwa haki na utu wao haviuzwi
Feb 12, 2026 07:53Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa umati mkubwa wa wananchi wa walioshiriki katika maandamano ya kitaifa ya kuadhimisha kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 wametangaza wazi kwamba haki na utu wao haviuzwi.
-
Maandamano ya tarehe 22 Bahman, ishara ya mwamko, kuwa macho, umoja na mshikamano wa watu wa Iran.
Feb 12, 2026 03:09Ikiwa ni katika kuadhimisha mwaka wa 47 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, maandamano ya tarehe 22 Bahman sawa na tarehe 11 Februari yamefanyika mjini Tehran sambamba na miji mingine mingi, yakiushirikisha umati mkubwa wa watu katika pembe zote za nchi.
-
Admeri Shamkhani asisitiza: Mpango wa makombora wa Iran hautajadiliwa katu
Feb 12, 2026 03:01Uwezo wa makombora ya balestiki ya Iran ni "mstari mwekundu" ambao hautawekwa katu kwenye meza ya mazungumzo. Hayo yameelezwa na afisa wa ngazi ya juu wa ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Viongozi wa dunia watoa salamu za pongezi kwa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 11, 2026 23:36Viongozi wa nchi mbalimbali wametuma jumbe kwa Rais wa Iran wakimpongeza kwa mnasaba wa Siku ya Taifa ya Iran na ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Azimio la maandamano ya Bahman 22: Tunaunga mkono kwa 100% diplomasia na medani ya kijeshi
Feb 11, 2026 10:30Wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliohudhuria maandamano ya Bahman 22 mjini Tehran wameidhinisha azimio la maandamano hayo na kutangaza kwamba, sasa ni wakati wa ushirikiano kati ya medani ya kijeshi na ya diplomasia, na kwamba askari wa nyuga zote hizo mbili wanatokana na kizazi cha taifa na wanaungwa mkono kwa asilimia mia moja na wananchi wa Iran.
-
Pezeshkian: Dunia ishuhudie jinsi Wairani walivyojitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya Bahman 22 ili kuihami nchi yao
Feb 11, 2026 06:00Rais Masoud Pezeshkian amesema kuwa dunia inapasa kuona jinsi mailioni ya wananchi wa Iran walivyomiminika mitaani katika maandamano ya mamilioni ya wananchi kote nchini ili kulinda mapinduzi yao, kutii uongozi wa mfumo, na kutetea thamani na nchi yao ya kujivunia.
-
Mamilioni wamiminika mitaani Iran kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 11, 2026 03:38Mamilioni ya wananchi kutoka matabaka yote ya kijamii wamejitokeza mitaani kote nchini Iran kushiriki maandamano ya kitaifa yanayoashiria maadhimisho ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Iran yaonya kuhusu njama za Israel huku ikiendeleza mazungumzo ya kidiplomasia na Marekani
Feb 10, 2026 23:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametoa tahadhari kuhusu azma ya utawala wa Israel ya kuishawishi Marekani iingie katika vita vingine dhidi ya Iran, wakati mazungumzo mapya ya nyuklia kati ya Tehran na Washington yakiwa yameanza.