-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu la Iran kusimama kidete kuhusu suala la nyuklia
Feb 23, 2021 08:28Kama ilivyo hali kuhusu masuala mengine, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitalegeza msimamo wake kuhusu kadhia ya nyuklia, na itaendelea kusimamam imara na kutetea suala hilo kwa nguvu zake zote kwa ajili ya kulinda maslahi ya leo na ya kesho ya taifa hili.
-
Raisi: Marekani na Wamagharibi zimekanyaga haki za binadamu katika vita vya kulazimishwa
Feb 23, 2021 04:22Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesisitiza kuwa, Marekani na Wamagharibi walikanyaga haki za binadamu katika vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na utawala wa Saddam dhidi ya Iran.
-
Iran imeanza kupunguza kiwango cha ushirikiano inaotoa kwa IAEA
Feb 23, 2021 01:31Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika taasisi za kimataifa huko Vienna, Austria, amesema leo Iran imeanza kutekeleza sheria ya "hatua za kistratijia kwa ajili ya kuondolewa vikwazo na kulinda haki za taifa la Iran." Kwa mujibu wa sheria hiyo, kuanzia Februari 23 Iran inasitisha utekelezwaji wa protokali ziada na hivyo Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA hautakuwa na idhini kamili ya kukagua vituo vyake vya nyuklia.
-
Ayatullah Khamenei: Urutubishaji madini ya urani nchini yumkini ukafikia asilimia 60 kulingana mahitaji ya taifa
Feb 22, 2021 14:37Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitalegeza kamba katika misimamo yake ya kimantiki kwenye maudhui ya nyuklia na itarutubisha madini ya urani hata kufikia asilimia 60 kulingana na maslahi na mahitaji ya nchi.
-
Baada ya kubwagwa Trump; Iran na Korea Kusini zafikia makubaliano ya kuhamishiana fedha za kigeni
Feb 22, 2021 10:36Gavana wa Benki Kuu ya Iran na balozi wa Korea Kusini hapa Tehran wamekutana katika kikao kilichopendekezwa na balozi wa Korea Kusini, na pande mbili zimefaikiana juu ya namna ya kukabidhiana fedha na matumizi ya vyanzo vya kibenki vya Iran huko Korea Kusini.
-
Khatibzadeh: Iran haijafanya mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani
Feb 22, 2021 04:34Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hakujafanyika mazungumzo ya moja kwa moja baina ya taifa hili na Marekani na kwamba, maelezo yanayobainishwa na kuonyesha kama kumekuweko na mazungumzo ya moja kwa moja baina ya Tehran na Washington hayana ukweli wowote.
-
Wabunge wa Iran wasisitiza ulazima wa kusimamishwa utekelezaji wa hiari wa Protokali ya Ziada
Feb 21, 2021 23:26Wabunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran wamesisitiza katika taarifa kwamba utekelezaji wa hiari wa Protokali ya Ziada ya Mkataba unaopiga marufuku uundaji na uenezaji wa silaha za nyuklia NPT utasimamishwa.
-
Zarif alaani unafiki wa Marekani na Ulaya kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA
Feb 21, 2021 13:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Marekani na Ulaya zinafanya unafiki katika mienendo yao kuhusiana na makubalino ya nyuklia ya Iran maarufu kwa kifupi kama JCPOA.
-
Chanjo ya corona ya Iran kuingia awamu ya pili ya majaribio kwa wanadamu
Feb 21, 2021 12:59Kundi la utafiti wa chanjo ya virusi vya corona ya Iran inalojulikana kwa jina la 'COVO-Iran Barakat' limetangaza kuwa chanjo hiyo iko tayari kwa ajili ya awamu ya pili ya majaribio kwa wanadamu.
-
Iran: Muhula wa kusimamisha 'Protokali ya Ziada' unakaelekea kumalizika
Feb 21, 2021 04:24Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa ameonya kuwa, iwapo Marekani haitachukua hatua yoyote ya kuliondolea vikwazo taifa hili kufikia kesho kutwa (Februar 23), basi Tehran itachukua hatua ya kusimamisha Protokali ya Ziada ya kupunguza kiwango cha uangalizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).