-
Iran: Muhula wa kusimamisha 'Protokali ya Ziada' unakaelekea kumalizika
Feb 21, 2021 04:24Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa ameonya kuwa, iwapo Marekani haitachukua hatua yoyote ya kuliondolea vikwazo taifa hili kufikia kesho kutwa (Februar 23), basi Tehran itachukua hatua ya kusimamisha Protokali ya Ziada ya kupunguza kiwango cha uangalizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).
-
Admeri Sayyari: Adui anaogopa uwezo wa kujihami wa Iran
Feb 21, 2021 04:19Naibu Mratibu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema adui anatiwa hofu na uwezo mkubwa wa kiulinzi wa taifa hili akifahamu fika kuwa, iwapo atajaribu kufanya kosa lolote, basi atakabiliwa kwa jibu kali.
-
Kiongozi Muadhamu asifu nafasi ya vijana katika masuala muhimu ya nchi
Feb 20, 2021 10:09Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepongeza nafasi ya kipekee ya tabaka la vijana katika masuala muhimu nchi na kueleza kuwa, uwepo wa kizazi hicho katika masuala hasasi ya nchi ni katika mafanikio na fakhari ya Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Khatibzadeh: Ili kuhuisha JCPOA, ni dharura Marekani kuondoa kivitendo vikwazo dhidi ya Iran
Feb 19, 2021 23:44Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema njia pekee ya kuhuisha mapatano ya nyuklia ya JCPOA ni Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Iran.
-
Chanjo ya Corona ya Sputnik V ya Russia kuanza kutegenezwa Iran
Feb 19, 2021 23:36Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa, chanjo ya Corona au COVID-19 ya Sputnik V ya Russia sasa itaanza kutengenezwa hapa nchini.
-
Zarif: Marekani inapaswa kuondoa bila masharti yoyote vikwazo vyote vilivyowekwa na Trump
Feb 19, 2021 10:38Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Marekani inapaswa kuondoa bila masharti yoyote na kwa namna iliyo athirifu vikwazo vyote vilivyorejeshwa upya na kutekelezwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Donald Trump.
-
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu; sisitizo la "kuimarishwa vielelezo vya utambulisho na "kuongezwa nguvu za ndani"
Feb 18, 2021 06:27Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumatano ya jana tarehe 17 Februari alibainisha matunda na mafanikio makubwa ya Mapinduzi ya Kiislamu katika hotuba yake aliyoitoa kwa njia ya mawasiliano ya intaneti kwa mnasaba wa kumbukumbu ya harakati na mapambano ya kihistoria na yasiyosahaulika ya wananchi wa mji wa Tabriz ya 29 Bahman 1356 (Februari 1978).
-
Rouhani: serikali ya Marekani haina njia nyingine ghairi ya kusalimu amri mbele ya sheria
Feb 18, 2021 05:58Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa, leo hii Marekani na serikali mpya ya nchi hiyo zimetambua kuwa zilifanya makosa kuhusu Iran na kueleza kuwa: Kusalimu amri mbele ya sheria si aibu na kwamba serikali ya Marekani haina njia nyingine ghairi ya kusalimu amri mbele ya sheria.
-
Rouhani: Haiyumkiniki kujumuisha maudhui nyingine katika JCPOA
Feb 17, 2021 23:44Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ni jambo lisilowezekana kuarifisha na kujumuisha maudhui nyinginezo katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Zarif: Kuanzia Februari 23 Iran itapunguza uangalizi wa IAEA kwa shughuli zake za nyuklia
Feb 17, 2021 08:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu inaendeleza mashirikiano yake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, lakini kuanzia tarehe 23 Februari itapunguza usimamizi wa wakala huo kwa shughuli zake za nyuklia.