-
Zarif: Kuanzia Februari 23 Iran itapunguza uangalizi wa IAEA kwa shughuli zake za nyuklia
Feb 17, 2021 08:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu inaendeleza mashirikiano yake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, lakini kuanzia tarehe 23 Februari itapunguza usimamizi wa wakala huo kwa shughuli zake za nyuklia.
-
Rais Rouhani: Iran haina mpango wa kutumia silaha za maangamizi ya umati
Feb 17, 2021 04:37Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi hii haijawahi kuwa na mpango wa kumiliki silaha za nyuklia wala kuzitumia.
-
Zarif: Matukio ya kimataifa hayaathiri uhusiano wa kistratijia wa Iran-China
Feb 16, 2021 22:57Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amepongeza 'ushirika wa kistratijia' wa Iran na China na kuongeza kuwa, matukio ya kimataifa hayawezi kuathiri urafiki baina ya washirika hawa wawili.
-
Admeri Khanzadi: India itajiunga na mazoezi mseto ya kijeshi ya Iran na Russia katika Bahari ya Hindi
Feb 16, 2021 22:56Kamanda wa Jeshi Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema lengo kuu la mazoezi mseto ya usalama wa baharini katika eneo la kaskazini mwa Bahari ya Hindi ni kufikia usalama jumla kieneo. Aidha ameongeza kuwa, Jeshi la Majini la India sasa litajiunga na majeshi ya majini ya Iran na Russia katika mazoezi hayo.
-
Ayatullah Khamenei: Tutatekeleza makubaliano ya JCPOA iwapo upande wa pili utayatekeleza
Feb 17, 2021 08:09Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ameashiria hotuba yake ya hivi karibuni kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA baina ya Iran na nchi tano za kundi la 5+1 na kusema kuwa: Iwapo upande mwingine utatekeleza makubaliano hayo, Iran pia itatekeleza vipengee vyake, na mara hii Jamhuri ya Kiislamu haitatosheka kwa maneno na ahadi tupu.
-
Amani na urafiki, ndio ujumbe muhimu zaidi wa mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya baharini ya Iran na Russia
Feb 16, 2021 09:21Msemaji wa mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya baharini ya ukanda wa amani 2021 yanayoshirikisha majeshi ya Iran na Russia amesema, mazoezi hayo yanyaoanza leo yanafanyika kwa kufuata kalenda ya kila mwaka ya nchi washiriki; na ujumbe wake muhimu zaidi ni amani na urafiki.
-
IRGC: Israel itapata jibu kwa jinai zake dhidi ya taifa la Iran
Feb 16, 2021 04:32Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema hakuna chembe ya shaka kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel utapokea jibu kali la Iran kutokana na jinai zake dhidi ya taifa hili, yakiwemo mauaji ya wanasayansi na wasomi wa Iran.
-
Rouhani: Usalama na amani ya Asia Magharibi vitaimarishwa kupitia ushirikiano wa nchi za eneo
Feb 16, 2021 00:05Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema amani na usalama katika eneo la Asia Magharibi vinaweza kuimarishwa tu kupitia ushirikiano wa mataifa ya eneo hili na wala si kwa uingiliaji wa madola ajinabi.
-
Namaki: Iran itakuwa mmoja wa wazalishaji wakubwa wa chanjo ya corona duniani
Feb 15, 2021 09:48Waziri wa Afya wa Iran amesema kuwa hadi miezi mitatu ijayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakuwa miongioni mwa wazalishaji wakubwa wa chanjo ya corona duniani.
-
Majeshi ya Iran na Russia kufanya mazoezi makubwa ya kivita Bahari ya Hindi
Feb 14, 2021 10:16Majeshi ya Majini ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia yatafanya mazoezi ya pamoja ya kivita kaskazini mwa Bahari ya Hindi. Hayo yamedokezwa na Admeri Habibullah Sayyari, Mratibu Mkuu wa Majeshi ya Iran ambaye ameongeza kuwa: "Kufanyika mazoezi hayo ni dhihirisho la nguvu za Majeshi ya Iran."