-
Silaha za nyuklia za Israel ni tishio kwa usalama wa dunia
Sep 27, 2020 01:12Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa utawala wa Kkizayuni wa Israel unaomiliki makumi ya makombora ya nyuklia ndio tishio kubwa zaidi la amani na usalama wa eneo la magharibi mwa Asia.
-
Kurejea kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA, hatua ya kwanza inayopasa kuchukuliwa na Marekani
Sep 27, 2020 00:38Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akiyataja mapatano ya nyuklia ya JCPOA kuwa ndiyo mapatano mabaya zaidi kwa nchi yake na hatimaye mwezi Mei mwaka 2018 aliiondoa nchi hiyo kwenye mapatano hayo na kuiwekea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo vikali. Hivi sasa Joe Biden mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Democratic huko Marekani amesema iwapo atashinda uchaguzi huo wa mwezi Novemba mwaka huu atairejesha Marekani katika mapatano hayo ya JCPOA.
-
Rouhani: White House ni mhusika wa jinai zote dhidi ya taifa la Iran
Sep 26, 2020 08:49Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Ikulu ya White House ya Marekani ndilo chimbuko la jinai zote dhidi ya binadamu, mashinikizo na vikwazo visivyo vya kiutu dhidi ya wananchi wa Iran.
-
Taarifa ya Umoja wa Ulaya dhidi ya Iran; mwendelezo wa misimamo ya kindumakuwili kuhusu haki za binadamu
Sep 26, 2020 06:50Nchi za Magharibi zimekariri tena madai yao ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Iran wakati idadi kubwa ya nchi hizo, kama Ufaransa na Uingereza, zimewekwa kwenye orodha ya wakiukaji wa haki hizo za binadamu.
-
Zaidi ya wagonjwa 3,000 wapya wa corona wagunduliwa nchini Iran
Sep 25, 2020 07:45Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran ametangaza kuwa, zaidi ya wagonjwa wapya elfu tatu (3,000) wa COVID-19 wamegunduliwa humu nchini katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.
-
Ukurasa mpya wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Iran na Afghanistan
Sep 25, 2020 03:06Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Afghanistan upo katika mkondo wa kupiga hatua na katika uwanja huo, na kwa mara ya kwanza kumefanyika maonyesho ya kitaalamu ya Iran kwa muda wa siku tatu katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul.
-
Brigedia Jenerali Dehqan: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalitoa pigo la kihistoria dhidi ya Marekani
Sep 24, 2020 08:33Mshauri wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran katika masuala ya sekta ya viwanda vya ulinzi amesema kuwa, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuwa pigo kubwa zaidi la kihistoria dhidi ya Marekani na yaliinasua nchi hii kutoka katika makucha ya ukoloni wa Magharibi.
-
Kamanda Fadavi: Marekani haitoweza kuunda muungano dhidi ya Iran
Sep 23, 2020 23:12Kaimu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, njama za Marekani za kuunda muungano ulio dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zitashindwa tu.
-
Rouhani: tuhuma na mahesabu ghalati ya Saddam zinakaririwa leo na Marekani
Sep 23, 2020 09:56Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria vita vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Iran na kusema: tuhuma na mahesabu ghalati ya viongozi wa White House yanafanana na hatua zilizochukuliwa na utawala wa Saddam na kupelekea kuangamizwa utawala huo.
-
Kubainisha utambulisho halisi wa Marekani; mhimili wa hotuba ya Rais Rouhani katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Sep 23, 2020 06:23Mwaka huu mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unafanyika katika mazingira maalumu kutokana na kuenea ulimwenguni kote virusi vya corona.