Silaha za nyuklia za Israel ni tishio kwa usalama wa dunia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i63664-silaha_za_nyuklia_za_israel_ni_tishio_kwa_usalama_wa_dunia
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa utawala wa Kkizayuni wa Israel unaomiliki makumi ya makombora ya nyuklia ndio tishio kubwa zaidi la amani na usalama wa eneo la magharibi mwa Asia.
(last modified 2026-08-14T10:24:44+00:00 )
Sep 27, 2020 01:12 UTC
  • Silaha za nyuklia za Israel ni tishio kwa usalama wa dunia

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa utawala wa Kkizayuni wa Israel unaomiliki makumi ya makombora ya nyuklia ndio tishio kubwa zaidi la amani na usalama wa eneo la magharibi mwa Asia.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran iliyotolewa jana kupitia mtandao wa Twitter kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Kuangamiza Silaha za Nyuklia (26 Septemba) imesema, siku hiyo ni fursa nzuri kwa jamii ya kimataifa kwa ajili ya kutazama upya majukumu yake ya kuangamiza silaha za nyuklia na kulipa suala hilo kipaumbele zaidi. 

Ujumbe huo umesema kuwa: Iran inaamini suala la kuwepo ulimwengu wenye amani na usalama na usio na silaha za mauaji ya halaiki.

Ujumbe wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran umeongeza kuwa, hatua ya utawala wa Marekani ya kupuuza makubaliano ya kimataifa na mipango ya nchi hiyo ya kuzalisha silaha mpya za nyuklia vinaitumbukia dunia katika ushindani mpya wa silaha. 

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran pia imeashiria kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unaomiliki makumi ya mabomu ya nyuklia ndio tishio kubwa zaidi la usalama eneo la magharibi mwa Asia na kuongeza kuwa, Israel ikisaidiwa na Marekani inazuia jitihada za kuifanya Asia Magharibi kuwa eneo lisilo na silaha za nyuklia.