-
Rouhani: Kutengwa zaidi, matunda ya mashinikizo ya juu zaidi ya Marekani dhidi ya Iran
Sep 20, 2020 23:47Rais Hassan Rouhani ameashiria kuhusu kugonga mwamba njama za Marekani dhidi ya taifa la Iran na kueleza bayana kuwa: Hatua za Washington mkabala wa Iran hazijakuwa na matokeo mengine isipokuwa kuifanya nchi hiyo itengwe zaidi katika uga wa kimataifa.
-
Khatibazadeh: Marekani inajua madai yake ya vikwazo dhidi ya Iran ni hewa
Sep 20, 2020 22:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amesema tangazo la Marekani kwamba vikwazo vyote vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Tehran ambavyo vilikuwa vimeondolewa eti vimerejeshwa upya ni madai hewa, yasio na athari yoyote na yaliyo kinyume cha sheria.
-
Iran: Marekani ndiye mhatarishaji mkubwa wa usalama na amani duniani
Sep 20, 2020 06:59Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumapili imetoa tamko rasmi na kusema kuwa, Marekani ndiye mhatarishaji mkubwa wa usalama na amani katika kona zote za dunia.
-
Zaidi ya wagonjwa 3000 wengine wa corona wagunduliwa nchini Iran
Sep 20, 2020 06:56Msemaji wa Wizara ya ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran ametangaza kuwa, zaidi ya wagonjwa wapya elfu tatu (3,000) wa COVID-19 wamegunduliwa humu nchini; na wagonjwa 183 wamefariki dunia kwa ugonjwa huo hatari katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.
-
Madai ya Marekani kuhusu kurejeshwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran; ndoto na kujidanganya kwake
Sep 20, 2020 05:56Kugonga mwamba Marekani katika juhudi zake za kutaka muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran uongezwe katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuliifanya serikali ya Donald Trump sambamba na kuibuka na madai kuwa, ni mwanachama wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kwamba, Iran imekiuka makubaliano hayo, ilidai kurejea upya vikwazo vya kimataifa dhidi ya Tehran na ikatoa muhula wa mwezi mmoja katika uwanja huo
-
Balozi wa Iran UN: Muhula bandia iliotoa Marekani umeshapita na vikwazo havijarudi tena upya
Sep 20, 2020 03:17Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameashiria madai ya Marekani ya kurejesha tena vikwazo vilivyofutwa na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa na kusisitiza kwamba muhula bandia iliotoa Marekani umeshapita na vikwazo hivyo havijarudi tena upya.
-
Ulyanov: Jamii ya kimataifa imepuuza madai ya Marekani dhidi ya Iran
Sep 19, 2020 22:09Mwakilishi wa Russia katika jumuiya za kimataifa mjini Vienna ameunga mkono barua iliyotumwa na Troika ya Ulaya katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la kusitishwa vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran na kusema jitihada zinazofanywa na Marekani kwa ajili ya kurefusha muda wa vikwazo hivyo hazina mashiko wala mantiki.
-
Vyombo vya Usalama Afrika Kusini: Hakuna ushahidi wa madai ya US dhidi ya Iran
Sep 19, 2020 08:26Idara ya Usalama wa Taifa ya Afrika Kusini imesema hakuna ushahidi wowote iliyoupata wa madai ya Marekani kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapanga kumuua Lana Marks, Balozi wa Marekani katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
-
Jenerali Salami: Kisasi cha Iran kwa mauaji ya Soleimani kitawalenga wahusika
Sep 19, 2020 08:23Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema hakuna chembe ya shaka kwamba Iran italipiza kisasi cha kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH.
-
Afrika Kusini yakadhibisha tuhuma za Marekani dhidi ya Iran
Sep 19, 2020 06:34Baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, serikali ya Rais Donald Trump ilizidisha mashinikizo ya kiwango cha juu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa shabaha ya eti kulemaza uchumi wa Iran na imekuwa ikitumia kila liwezekanalo kuanzisha vita vya kinafsi na kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kutoa vitisho dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.