-
Gharib Abadi: Saudia inafuata mkondo ule ule wa Wazayuni katika miradi yake ya nyuklia
Sep 19, 2020 03:01Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Taasisi za Kimataifa zenye makao yao mjini Vienna Austria amesema katika kikao cha jana cha Bodi ya Magavana wa Wakala wa Kimataifa wa Nishatia ya Atomiki IAEA kwamba Saudi Arabia si muwazi katika shughuli zake za nyuklia na ameitaka bodi hiyo kuishinikiza Riyadh kuheshimu mipaka na ahadi zake katika suala hilo.
-
Iran: Njia yoyote ya uchukuaji hatua inayopuuza matakwa ya taifa la Palestina ni batili
Sep 19, 2020 00:03Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetangaza kuwa: Njia yoyote ile ya uchukuaji hatua ikiwemo ya "Muamala wa Karne" ambayo haitatilia maanani matakwa ya taifa la Palestina ni batili.
-
Waziri Zarif amjibu Pompeo: Hakuna kitu kipya kitakachofanyika Septemba 20
Sep 18, 2020 03:39Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu matamshi ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo juu ya njama za Washington za kutaka kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran kwa kutumia mchakato unaofahamika kama 'Snapback Mechanism' na kusisitiza kuwa, 'Hakuna kitu maalumu kitakachofanyika Jumapili ya Septemba 20.'
-
Spika wa Bunge la Iran: Watawala wasaliti Asia Magharibi ni washirika wa jinai zote za Wazayuni
Sep 17, 2020 22:14Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu Asia Magharibi ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusema kuwa, watawala wasaliti Asia Magharibi ni washirika wa jinai zote za Wazayuni za huko nyuma mpaka sasa.
-
Gharib Abadi: Shughuli za nyuklia za Iran zina uwazi zaidi kuliko za nchi nyingine zote wanachama wa IAEA
Sep 17, 2020 08:46Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika mashirika ya kimataifa yenye makao yao mjini Vienna amesema asilimia 22 ya ukaguzi wote uliofanywa duniani na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA imefanyiwa Iran na akaeleza kwamba Tehran ndiyo inayoendesha kwa uwazi zaidi shughuli zake za nyuklia zenye malengo ya amani kuliko nchi zote wanachama wa wakala huo.
-
Shamkhani amwambia Trump: Wanaowaua Wairani watapelekwa jongomeo
Sep 17, 2020 03:41Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amejibu vitisho vilivyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran na kusema: Wanaoamuru na watekelezaji wa mauaji ya wana wa Iran kama diteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein na wengineo, watapelekwa jongomeo.
-
Kikao cha Kimataifa cha Mwamko wa Kiislamu cha Tehran; shabaha na majukumu ya kukabiliana na usaliti wa malengo ya Palestina
Sep 16, 2020 21:53Utawala mtenda jinai wa Kizayuni ambao umepandikizwa katika kitovu cha ulimwengu wa Kiislamu kwa jinai, uporaji na kuzikalia kwa mabavu ardhi za Waislamu, hauwezi kupata uhalali wa aina yoyote ile hata kukifanyika njama za kila namna.
-
Iran: Makubaliano yoyote hayatodumu mpaka yatekeleze sawa haki na majukumu
Sep 16, 2020 21:52Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya haki za kimataifa amesema kuwa, makubaliano yoyote yale ya kimataifa hayawezi kudumu bila ya kuweko mlingano sawa katika utekelezaji wa haki na majukumu, na kwamba mapatano ya nyuklia ya JCPOA nayo hayawezi kutoka kwenye msingi huo.
-
Rais Rouhani: Marekani imefeli katika jitihada zake za kutaka kutumia 'Utaratibu wa kifyatuo'
Sep 16, 2020 06:49Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani imefeli na kushindwa katika juhudi zake za kutaka kutumia utaratibu wa kusuluhisha mzozano katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, unaojulikana kama 'Utaratibu wa Kifyatuo' kwa kimombo "Trigger Mechanism".
-
Propaganda za kihabari na kisiasa za nyuma ya pazia dhidi ya Iran
Sep 16, 2020 03:31Senario ya kuenea chuki dhidi ya Iran “Iranophobia” hadi sasa zimeendeshwa kwa kutumia maudhui mbalimbali kama uingiliaji wa Iran katika masuala ya ndani ya nchi nyingine katika eneo la Asia Magharibi, tishio la Tehran la nguvu za kijeshi, makombora na kuunga mkono ugaidi, ukiukaji wa haki za binadamu na kuzusha wasiwasi katika uga wa miradi ya nyuklia ya Iran inayofanyika kwa malengo ya amani.