-
Iran yatengeneza kipimo cha haraka cha kinga ya mwili ya corona (antibodi)
Apr 12, 2020 03:16Mkuu wa Kituo cha Uhusiano wa Umma na Upashaji Habari cha Wizara ya Afya na Tiba ya Iran amesema kuwa tayari nchi hii iimetengeneza kipimo cha antibodi yaani kinga ya mwili ya Covid-19 na kipimo cha haraka cha corona (rapid test) kwa ajili ya kutambua antibodi.
-
Watu karibu 42,000 wapona corona Iran, milioni 1.7 waathiriwa kote duniani
Apr 11, 2020 10:36Huku idadi ya kesi mpya za ugonjwa wa Covid-19 (corona) ikiendelea kushuka kwa siku kadhaa sasa nchini iran, kufikia leo mchana watu karibu 42,000 walikuwa wamesharuhusiwa kurudi nyumbani kutoka mahospitalini baada ya kupata nafuu kikamilifu.
-
Mtihani wa Corona wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa; kwa maslahi au dhidi ya Iran
Apr 10, 2020 23:51Akijibu hatua za kibaguzi za Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) wakati huu mgumu wa maambukizi ya corona, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mfuko huo unapasa kutekeleza majukumu yake.
-
Zaidi ya watu 35,000 wapata afueni ya corona nchini Iran
Apr 10, 2020 07:31Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Matibabu ya Iran imetangaza kuwa, kasi ya mchakato wa kuzidi kupata afya njema na afueni kutokana na Corona imeongezeka sana humu nchini kiasi kwamba, hadi leo mchana watu 35 elfu na 465 walisharuhusiwa kurudi nyumbani kutoka mahospitalini baada ya kupata nafuu kikamilifu.
-
Amir Abdollahian: Mbali na vikwazo, sasa Marekani inafanya uharamia wa vifaa vya corona
Apr 09, 2020 22:01Mshauri wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, mbali na kuziwekea nchi mbalimbali vikwazo, Marekani hivi sasa inafanya pia uharamia wa kupora shehena za barakoa (mask) na vifaa vya kupimia ugonjwa wa COVID-19 duniani.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu; kung’ara taifa la Iran katika mtihani wa virusi vya Corona
Apr 09, 2020 08:46Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, taifa la Iran limeng’ara na kufaulu vizuri katika mtihani mgumu wa virusi vya Corona, hata hivyo kilele cha fahari ni mali ya wafanyakazi wa sekta ya tiba na afya.
-
Kiongozi Muadhamu: Hitajio la mwanadamu wa leo kwa mkombozi ni nadra kuwahi kushuhudiwa katika historia
Apr 09, 2020 08:41Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hitajio la kina na pana la mwanadamu wa leo la kuwa na mkombozi ni nadra kushuhudiwa katika historia. Amesisitiza kuwa, maana halisi na yenye manufaa ya kusubiri mwokozi ni kuwa na matumaini na itikadi kuhusu faraja sambamba na kuchukua hatua za kufikia mustakbali mwema na akaongeza kuwa: "Taifa la Iran limefaulu vizuri katika mtihani wa ugonjwa wa hivi karibuni; na mwenendo na nidhamu ya umma ni nzuri katika kufuata maelekezo."
-
Kiongozi Muadhamu alipongeza taifa la Iran kwa kukabiliana na janga la corona
Apr 09, 2020 03:53Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelipongeza taifa la Iran kwa jitihada zake za dhati za kupambana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona, huku akilitaja janga hilo kama mtihani unaoikabili dunia nzima.
-
Iran kurutubisha urani hadi SWU milioni moja iwapo EU itafeli kutoa dhamana ya kutekeleza JCPOA
Apr 09, 2020 03:52Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) imesema Tehran itaendelea kurutubisha urani kwa kiwango inachotaka, lakini inaweza kuangalia upya urutubishaji huo iwapo tu Umoja wa Ulaya utatoa dhamana ya kivitendo ya kuheshimu na kufungamana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Iran yaungana na ulimwengu wa Kiislamu katika maadhimisho ya kukumbuka kuzaliwa Imam Mahdi (AF)
Apr 08, 2020 23:27Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeungana na ulimwengu wa Kiislamu hii leo kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Mahdi (AF).