-
Iran yasikitishwa na ukandamizaji dhidi ya Waislamu nchini India
Mar 02, 2020 09:59Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza masikitiko yake kuhusiana na ukandamizaji wanaofanyiwa Waislamu nchini India na kusema kuwa, Tehran inaitambua India kuwa ni nchi ya kuvumiliana kidini; hivyo habari za kuwepo ukandamizaji dhidi ya Waislamu nchini humo ni suala linalotia wasiwasi mkubwa.
-
Zarif: Marekani imesalimu amri baada ya idhilali iliyopata kwa miaka 19 nchini Afghanistan
Mar 02, 2020 04:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuhusu kusainiwa mkataba wa suluhu kati ya kundi la Taliban na Marekani, kwamba hivi sasa na baada ya kudhalilishwa kwa muda wa miaka 19, Marekani imewasilisha pendekezo la kusalimu amri nchini Afghanistan.
-
Iran: Marekani inafanya njama za kuhalalisha uvamizi wake Aghanistan; amani ya kudumu itapatikana kwa makubaliano ya Waafghani wenyewe
Mar 01, 2020 08:31Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa kuhusu makubaliano yaliyotiwa saini jana Jumamosi baina ya Marekani na kundi la Taliban la Afghanistan na kusisitiza kuwa, amani ya kudumu nchini humo itapatikana tu kupitia mazungumzo ya Waafghani wenyewe kwa wenyewe na kushirikishwa makundi yote likiwemo la Taliban.
-
Mamia waandamana katika miji ya US kulaani mauaji ya Waislamu India
Mar 01, 2020 04:26Mamia ya raia wa Marekani wenye asili ya India wamefanya maandamano katika miji mikubwa ya Marekani kulaani na kupinga ghasia zilizopelekea makumi ya watu kuuawa katika mji mkuu wa India, New Delhi.
-
Rais Rouhani asisitiza kuwa JCPOA itabakia hai kwa ushirikiano
Feb 29, 2020 23:39Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yataendelea kuwepo na kubakia hai madhali kutakuwepo na ushirikiano wa pande zote husika.
-
Mousavi ajibu kauli za kilaghai za Pompeo: Harakati za kimaonesho sio njia ya kupambana na corona
Feb 29, 2020 03:47Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, harakati za kimaonesho zinazofanywa kwa utashi wa kisiasa sio njia ya kupambana na kirusi cha corona.
-
Zarif: Vita dhidi ya Corona vitafanikiwa iwapo utakuwepo ushirikiano baina ya nchi zote
Feb 28, 2020 23:38Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na China wamefanya mazungumzo ya simu na kujadiliana suala zima la kuenea virusi hatari vya corona na njia za kupambana navyo.
-
Corona na jitihada za madaktari walioko mstari wa mbele wa kupambana na virusi visivyojali mipaka
Feb 28, 2020 08:55Wimbi la kuenea virusi hatari vya corona duniani sasa hivi limekuwa ndiyo daghadagha na wasiwasi mkubwa wa nchi zote huku jamii ya madaktari nchini Iran ikiwa mstari wa mbele kwa kufanya kazi usiku na mchana katika kupambana na virusi hivyo vinavyoenea kwa kasi.
-
Waziri wa Afya: Mapambano ya Iran dhidi ya virusi vya Corona yatawashangaza walimwengu
Feb 28, 2020 08:30Waziri wa Afya wa Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itaushangaza ulimwengu kutokana na mbinu yake ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.
-
Sala ya Ijumaa yaghairishwa katika mikoa 23 ya Iran kwa sababu ya mripuko wa kirusi cha corona
Feb 28, 2020 04:02Sala ya Ijumaa ya leo katika baadhi ya mikoa ya Iran imeghairishwa kutokana na mripuko wa kirusi cha corona.