Iran yasikitishwa na ukandamizaji dhidi ya Waislamu nchini India
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i59505-iran_yasikitishwa_na_ukandamizaji_dhidi_ya_waislamu_nchini_india
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza masikitiko yake kuhusiana na ukandamizaji wanaofanyiwa Waislamu nchini India na kusema kuwa, Tehran inaitambua India kuwa ni nchi ya kuvumiliana kidini; hivyo habari za kuwepo ukandamizaji dhidi ya Waislamu nchini humo ni suala linalotia wasiwasi mkubwa.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 02, 2020 09:59 UTC
  • Abbas Mousavi
    Abbas Mousavi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza masikitiko yake kuhusiana na ukandamizaji wanaofanyiwa Waislamu nchini India na kusema kuwa, Tehran inaitambua India kuwa ni nchi ya kuvumiliana kidini; hivyo habari za kuwepo ukandamizaji dhidi ya Waislamu nchini humo ni suala linalotia wasiwasi mkubwa.

Itakumbukwa kuwa baada ya kupasishwa sheria ya uraia nchini India, kuliongezeka vitendo vya ukandamizaji vinavyowalenga Waislamu nchini humo.

Katika uwanja huo Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kwa njia ya video, ameelezea matumaini ya kuhitimishwa haraka ukandamizaji huo dhidi ya Waislamu nchini India. Amesema matumaini hayo yanatokana na busara waliyonayo viongozi wa India. Mousavi ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafuatilia kwa wasiwasi habari za vita na hitilafu za kidini nchini India kupitia vyombo rasmi.

Waislamu nchini India wanapitia wakati mgumu kutokana na kukkandamizwa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amezungumzia upatanishi wa Tehran kati ya Uturuki na Syria na kusema kuwa, Iran inatambua mchakato wa mazungumzo ya Astana kuwa njia muhimu ya kutatua tofauti za Syria na itaendelea kufuatilia jambo hilo hadi kupatikane utulivu katika eneo hilo.

Vilevile amezungumzia uwepo wa Ufaransa katika eneo la Lango Bahari la Hormoz na kusema kuwa, uwepo wa majeshi ya kigeni katika eneo hilo unasababisha machafuko na ghasia na ni hatua zisizo sahihi. Akisisitiza kuwa uwepo wa askari wa kigeni ndio chanzo cha ukosefu wa usalama na machafuko katika eneo nyeti la Ghuba ya Uajemi, Msema wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa usalama wa eneo hili utapatikana tu kwa kushirikiana nchi majirani.

Akizungumzia makubaliano ya kundi la Taleban na Marekani Abbas Moussavi amesema, Iran inaamini kwamba amani itapatikana nchini Afghanistan kwa kuyashirikisha makundi mbalimbali chini ya uongozi wa serikali kuu ya Kabul.