-
Araqchi: Iran haitofanya tena mazungumzo kuhusu mapatano ya JCPOA
Sep 04, 2019 03:26Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya kisiasa amesema kuwa, Tehran inaamini kwamba hakuna mazungumzo mengine kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA, lakini yanaweza kuweko mazungumzo kuhusu utekelezaji kamili wa yaliyoafikiwa ndani ya mapatano hayo.
-
Zarif: Iran inaunga mkono ushiriki chanya wa Syria na Umoja wa Mataifa
Sep 03, 2019 08:41Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuhusu azma ya Tehran ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria kwa njia ya kisiasa na akasema Iran inaunga mkono ushiriki wowote chanya kati ya Damascus na Umoja wa Mataifa.
-
Makubaliano ya pande zote ya Iran na Russia; kuanzia kudhamini amani na usalama wa Ghuba ya Uajemi hadi kupanua ushirikiano wa kibiashara
Sep 03, 2019 06:17Sergei Lavrov, Waziri wa Mashauri yay Kigeni wa Russia alisema Jumatatu ya jana mbele ya waandishi wa habari mjini Moscow akiwa na mgeni wake, Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba, pande mbili hizo zimefikia makubaliano jumla.
-
Rais Rouhani: Iran haina ajenda ya kufanya mazungumzo na Marekani
Sep 03, 2019 03:25Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran haijawahi kuwa na ajenda ya kufanya mazungumzo ya pande mbili na Marekani.
-
Zarif: Iran itachukua hatua ya tatu ndani ya JCPOA kama ilivyopangwa hapo awali
Sep 02, 2019 22:38Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukua hatua ya tatu ya kupunguza utekelezaji wa majukumu yake ndani ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kama ilivyopangwa hapo awali na kwamba iwapo nchi za Ulaya hazitatekeleza majukumu yao ndani ya makubaliano hayo, Iran itatekeleza hatua hiyo ya tatu.
-
Mazungumzo ya Zarif mjini Moscow wakati huu wa kukaribia Iran kutekeleza awamu wa tatu ya kupunguza ahadi zake ndani ya JCPOA
Sep 02, 2019 22:36Dk Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelekea mjini Moscow, Russia kwa ajili ya kuonana na kuzungumza na waziri mwenzake wa nchi hiyo Sergey Lavrov kuhusu masuala muhimu wa pande mbili.
-
Rabiei: Stratejia ya Iran katika JCPOA ni pande zote mbili kuwajibika kwa kiwango sawa
Sep 02, 2019 08:47Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwajibika kwa kiwango sawa pande zote mbili katika kutekeleza majukumu, ndio stratejia na mkakati unaotumiwa na Tehran katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA; na akaongeza kuwa: Ikiwa Ulaya itatekeleza majukumu yake katika JCPOA, Iran nayo itarejea kwenye utekelezaji kamili wa makubaliano hayo.
-
Mousavi: Awamu ya tatu ya kupunguza Iran uwajibikaji wake kwenye JCPOA iko tayari kutekelezwa
Sep 02, 2019 03:13Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, awamu ya tatu ya kupunguza Jamhuri ya Kiislamu utekelezaji wa ahadi zake ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA iko tayari kutekelzwa na kusisitiza kuwa, kama juhudi za kidiplomasia za kuzuia jambo hilo hazitozaa matunda, Tehran bila ya shaka itaanza tu kutekeleza awamu hiyo ya tatu.
-
Zarif: Siku nne nyingine; muda wa kutangaza hatua ya tatu ya Iran ndani ya JCPOA
Sep 01, 2019 23:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa utekelezaji wa hatua ya tatu ya kupunguza ahadi na majukumu ya Iran kuhusiana na makubaliano ya JCPOA uko katika marhala ya mwisho ya uchukuaji maamuzi.
-
Iran yalaani shambulio la anga la Saudi Arabia lililolenga jela ya Al Maqsuf, Yemen
Sep 01, 2019 07:13Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali jinai mpya zilizofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia huko nchini Yemen.